180 – Abul-Qaasim ´Ubaydullaah bin Muhammad bin ´Ubaydillaah an-Najjaar ametukhabarisha: Muhammad bin ´Ubaydillaah bin al-Fadhwl al-Kayyaal ametukhabarisha: Muhammad bin al-Haytham al-Muqri’ ametuhadithia: Abu Sa´iyd al-Jassaasw amesema: Ibn ´Abdil-Mu’min ametuhadithia Misri: ´Abdaan bin ´Uthmaan ametuhadithia: Nimemsikia Ibn-ul-Mubaarak amesema:

Unapokuwa umepoa na umepumzika

chukua fursa ya kuswali Rak´ah mbili kwa ajili ya Allaah

na  pale unapofikiria kusema jambo la batili

basi badala yake mtukuze Allaah

181 – Abu Sa´iyd Mas´uud bin Naaswir as-Sijziy amenisomea: Abu Ahmad Mansuur bin Muhammad bin ´Abdillaah al-Azdiy amenisomea huko Herat:

Usidharau saa hata moja ya usaidizi

ambayo unanyoosha mkono katika utiifu

Aliye hai anapelekwa kwenye kifo – na kifo ni hadaa

Kila kitu ni kutoka saa kwenda saa nyingine

182 – Abul-Husayn ´Aliy bin Muhammad bin ´Abdillaah al-Mu-addil ametukhabarisha: al-Husayn bin Swafwaan ametuzindua: ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa ametuhadithia: Abu ´Abdillaah Ahmad bin Ayyuub alinisomea:

Tumia fursa ya wakati wako ijapo kwa Rukuu´ moja

Pengine mauti yako yakawa ghafla

Ni wazima wangapi nimewaona

Ambao wameondoka ghafla wakiwa wazima

183 – Abul-Waliyd Sulaymaan bin Khalaf bin Sa´d al-Andalusiy amenisomea:

Ikiwa najua kwa elimu yenye yakini kabisa

kwamba maisha yangu yote ni kama saa moja

Ni kwa nini basi nisiichunge

na kuitumia katika wema na utiifu?

184 – ´Aliy bin Ahmad ar-Razzaaz ametuhadithia: Nimemsikia Ja´far al-Khuldiy akisema: Nimemsikia al-Junayd akisema: Nimemsikia as-Sarriy as-Saqatwiy akisema:

Kila siku iliyopita

Kwa ajili hiyo itukuze kila siku unayokutana nayo

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 103-104
  • Imechapishwa: 26/05/2024