Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
1- Allaah (Ta´ala) amesema:
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُواْ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُواْ إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُواْ أَن يَكْفُرُواْ بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلاَلاً بَعِيدًا
”Je, huoni wale ambao wanadai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako, wanataka wahukumiane kwa Twaaghuut na hali wameamrishwa wakanushe hiyo, na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali kabisa.” (an-Nisaa´ 04:60)
2-
وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لاَ تُفْسِدُواْ فِي الأَرْضِ قَالُواْ إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ
”Na wanapoambiwa: “Msifanye uharibifu katika ardhi.” Husema: “Hakika sisi ni watengenezaji.” (al-Baqarah 02:11)
3-
وَلاَ تُفْسِدُواْ فِي الأَرْضِ بَعْدَ إِصْلاَحِهَا
”Na wala msifanye ufisadi katika ardhi baada ya kutengenea kwake.” (al-A´raaf 07:56)
4-
أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ
”Je, wanataka [uwahukumu kwa] hukumu ya kipindi cha makafiri?” (al-Maaidah 05:50)
5- ´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hatoamini mmoja wenu mpaka matamanio yake yawe ni yenye kufuata yale niliyokuja nayo.”[1]
an-Nawawiy amesema:
“Hadiyth ni Swahiyh. Nimeipokea katika “Kitaab-ul-Hujjah” kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.
6- ash-Sha´biy amesema:
“Kulikuwa ugomvi baina ya mtu mmoja mnafiki na mwingine myahudi. Yule myahudi akasema: “Twende kwa Muhammad atuhukumu.” Mnafiki yule alijua kuwa hachukui rushwa. Mnafiki yule akasema: “Twende kwa mayahudi watuhukumu.” Kwa kujua kwake kuwa wao wanachukua rushwa. Hivyo wote wawili wakakubaliana kumwendea kuhani Juhaynah ili awahukumu. Ndipo kukateremka:

Kuna maoni mengine yanayosema kwamba iliteremka juu ya watu wawili waliogombana ambapo mmoja wao akasema:
“Hebu tumpelekee kesi yetu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aihukumu.” Yule mwengine akasema: “Wacha tumpelekee Ka´b bin al-Ashraf.” Mwishowe wakampelekea nayo ´Umar mmoja wao akamueleza kisa kilivyokuwa. Akamuuliza yule ambaye hakuridhia ipelekwe kesi kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Mambo ni hivyo?” Mtu yule akasema: “Ndio.” ´Umar akampiga kwa upanga na akamuua.”
MAELEZO

”Je, huoni wale ambao wanadai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako, wanataka wahukumiane kwa Twaaghuut na hali wameamrishwa wakanushe hiyo, na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali kabisa.”
Anachotaka mwandishi ni kuwatahadharisha watu kuhukumiana kinyume na Shari´ah ya Allaah. Lililo la wajibu ni kuhukumian na Shari´ah ya Allaah katika mambo yote. Allaah (Ta´ala) amesema:
فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا
“Naapa kwa Mola wako! Hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni hakimu katika yale wanayozozana kati yao kisha wasipate katika nyoyo zao uzito katika yale uliyohukumu na wajisalimishe kwa kujisalimisha” (an-Nisaa´ 04:65)
وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ
“Wahukumu baina yao kwa yale aliyoyateremsha Allaah.” (al-Maaidah 05:49)
وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ
“Yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri.” (al-Maaidah 05:44)
وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ
“Yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio madhalimu.” (al-Maaidah 05:45)
وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ
“Yeyote asiyehukumu kwa yale aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio mafasiki.” (al-Maaidah 05:47)
Haya yote yanafahamisha juu ya uwajibu wa kuhukumiana na Shari´ah ya Allaah na kwamba haijuzu kuhukumiana na kitu kingine. Huu ni msingi ambao kuna maafikiano juu yake.
Aayah inabainisha vilevile kwamba wapo watu wanaodai imani na Uislamu ilihali ukweli wa mambo sivo hivyo; bali ni wanafiki. Kunapotokea kitu basi wanataka wahukumiwe kinyume na Shari´ah ya Allaah na Twaaghuut. Twaaghuut ni kila chenye kuabudiwa badala ya Allaah na mwenye kuhukumu kinyume na Shari´ah ya Allaah kwa kukusudia na kwa matamanio. Wanafiki wanataka wahukumiwe na yule ambaye anaafikiana na matamanio yao na ambaye anapokea rushwa ili aweze kuwapatia haki wao. Hii ni dalili juu ya unafiki wao. Wanafiki kazi yao ni kuipa mgongo haki. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ رَأَيْتَ الْمُنَافِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودًا
“Wanapoambiwa: “Njooni kwenye yale aliyoyateremsha Allaah na kwa Mtume”, basi utawaona wanafiki wanakugeukilia mbali kwa mkengeuko.” (an-Nisaa´ 04:61)
Kwa hivyo ni wajibu kwa mtu kutahadhari nao na tabia zao mbaya.

”Na wanapoambiwa: “Msifanye uharibifu katika ardhi.” Husema: “Hakika sisi ni watengenezaji.”
Wanadai kwamba ni wenye kutengeneza, lakini uhakika wa mambo ni wenye kuharibu kwa sababu ya ujinga wao, upotevu wao na unafiki wao. Akili zao zimepinduliwa chini juu na ndio maana wakachukulia ufisadi kuwa ni matengenezo. Kwa ajili hii Allaah (Ta´ala) akasema:
أَلَا إِنَّهُمْ هُمُ الْمُفْسِدُونَ وَلَـٰكِن لَّا يَشْعُرُونَ
“Tanabahi! Hakika wao ndio mafisadi lakini hawahisi.” (al-Baqarah 02:12)

”Na wala msifanye ufisadi katika ardhi baada ya kutengenea kwake.”
Kutengenea kwa ardhi kunakuwa kwa kufuata na kuhukumiana kwa Shari´ah. Inaharibiwa kwa kwenda kinyume na amri ya Allaah na kuhukumiana na sheria zengine.
4-
أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ
”Je, wanataka [uwahukumu kwa] hukumu ya kipindi cha makafiri?”
Watu hawa wanataka kuhukumiwa na mayahudi na Twaaghuut sampuli zengine kwa hukumu za kipindi cha kikafiri. Hivi kuna hukumu ilio bora kuliko hukumu ya Allaah? Yeye ndiye anajua bora manufaa ya waja Wake. Anajua namna mambo yatavyomalizika. Yeye ndiye mjuzi wa kila kitu.

“Hatoamini mmoja wenu mpaka matamanio yake yawe ni yenye kufuata yale niliyokuja nayo.”
Bi maana hatoamini imani kamilifu na ya wajibu mpaka matamanio yake, utashi wake, makusudio yake na matakwa yake yawe ni yenye kufuata yale aliyokuja nayo yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni wajibu makusudio ya muumini yawe ni yenye kujisalimisha na hukumu ya Allaah. Baadhi ya wanachuoni wamesema kuwa Hadiyth hii ni dhaifu, lakini hata hivyo maana yake ni sahihi.

Hii ni dalili inayoonyesha kuwa mnafiki ana shari zaidi kuliko myahudi. Kwa sababu wanawababaisha watu na kusababisha upotevu. Kwa ajili hio ndio maana wakawa katika tabala ya chini kabisa Motoni.
Ni wajibu kuhukumiana na Shari´ah ya Allaah na kutoridhia nyengine. Kisa cha ´Umar kinathibitisha kwamba kuhukumu kinyume na Shari´ah ni kufuru na kuritadi. Vilevile yule mwenye kuchukia hukumu ya Allaah ni kafiri. Usahihi wa visa vyote viwili unahitajia kutazamwa vizuri, lakini maana zake ni sahihi.
ash-Sha´biy ni ´Aamir bin Sharaahil.
Faida:
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah amemuumba Aadam kwa sura Yake.”[2]
Ina maana kwamba Allaah alimuumba Aadam kwa usikizi, uoni, akizungumza, uso, mikono, nyayo na mengineyo. Allaah anasikia na Aadam pia alikuwa akisikia. Allaah anazungumza na Aadam pia alikuwa akizungumza na kadhalika. Lakini hafanani na Allaah inapokuja katika dhati na sifa za Allaah:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (ash-Shuuraa 42:11)
Kuhusiana na ambaye amesema kuwa dhamiri inarudi kwa Aadam, ni kosa. Aliyesema hivo lengo lake ilikuwa kukimbia kufananisha.
[1] Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwilaal-ul-Jannah” (15)na ”Mishkaat-ul-Maswaabîh” (167).
[2] al-Bukhaariy (6227) na Muslim (2841).
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: harh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 124-126
- Imechapishwa: 31/10/2018

Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: harh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 124-126
Imechapishwa: 31/10/2018
https://firqatunnajia.com/39-mlango-maneno-yake-taala-je-huoni-wale-ambao-wanadai-kwamba-wao-wameamini-yaliyoteremshwa-kwako-na-yale-yaliyoteremshwa-kabla-yako-wanataka-wahukumiane-kwa-twaaghuut-na-hali-wam/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)