Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:
Fikira za wenye kufikiri haziwezi kumzunguka.Wafikiriaji wazingatie zile alama Zake, na wasifikirie juu ya dhati Yake.
MAELEZO
Namna yoyote utakayomfikiria Allaah (´Azza wa Jall), juu ya dhati Yake, matendo Yake, sifa na matendo Yake, basi hutofikia kikomo. Kilicho wajibu juu yako ni wewe kumwamini Allaah, majina na sifa Zake. Simama hapo. Usiulize juu ya namna.
Fikiria alama za Allaah; za kilimwengu na za kidini. Zingatia juu ya alama za kilimwengu kama vile ardhi, mlima, bahari, miti na mito. Zingatia kwamba vitu hivi vinajulisha juu ya uwepo wa Muumba. Mshairi anasema:
Ajabu iliyoje ni vipi Allaah anaasiwa
au ni vipi atakanushwa na wakanushwaji
ilihali katika kila kitu ipo alama
inayojulisha kuwa yeye ni Mmoja pekee
Pia fikiria juu ya alama za Allaah za kidini. Kwa msemo mwingine zizingatie, tafakari juu ya maana na tafsiri yake. Hata hivyo haijuzu kufikiria wala kuuliza ni namna gani Allaah amezungumza kwa Allaah au ni vipi anazungumza.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 33-34
- Imechapishwa: 31/07/2021
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)