Tambueni ya kwamba ni wajibu kubainisha vichenguzi vya swawm ili muislamu avijue na ajiepushe navyo na awe na tahadhari dhidi yake. Mambo haya yanayoharibu swawm yako katika aina mbili.
1 – Ni yale yanayoharibu swawm na kulazimisha kulipa siku.
2 – Ni yale yanayoharibu malipo ya swawm bila kulazimisha kulipa siku.
Ama mambo yanayobatilisha swawm na kulazimisha kulipa siku ni aina kadhaa.
1 – Jimaa.
Mtu yeyote mwenye kufunga akifanya jimaa mchana wa Ramadhaan, basi funga yake hubatilika. Inamlazimu ajizuilie kula na kunywa sehemu ya mchana uliyohaki. Aidha anapaswa atubie kwa Allaah na amwombe msamaha. Vilevile alipe siku hiyo aliyofanya jimaa. Pia inamlazimu kutoa kafara, nayo ni kuacha huru mtumwa. Asipompata mtumwa wa kumwacha huru, basi afunge miezi miwili mfululizo. Asipoweza kufunga miezi miwili mfululizo, basi awalishe chakula masikini sitini; kila masikini apewe nusu pishi ya ngano au chakula kingine kinachohesabika kuwa ni chakula katika desturi ya watu wa nchi hiyo.
Yule asiyeweza kufunga ni ambaye hana uwezo wa kufunga kwa sababu ya kizuizi kinachokubalika katika Shari´ah. Haina maana yule ambaye kufunga kunamletea uzito au mashaka tu. Dalili ya hilo ni ile iliyothibiti kwa al-Bukhaariy, Muslim na wengineo kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza:
“Wakati tulipokuwa tumekaa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuja mbedui mmoja akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Nimeangamia!” Akasema: “Ni kipi kilichokuangamiza?” Akajibu: “Nimemwingilia mke wangu katika Ramadhaan.” Ndipo Mtume wa Allaah akasema: “Unaweza kupata mtumwa ukamwacha huru?” Akajibu: “Hapana.” Akasema: “Unaweza kufunga miezi miwili mfululizo?” Akajibu: “Hapana.” Akasema: “Unaweza kupata chakula cha kuwalisha masikini sitini?” Akajibu: “Hapana.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akanyamaza. Tulipokuwa katika hali hiyo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaja na chombo kilicho na tende ambapo akauliza: “Yuko wapi muulizaji?” Akajibu: “Ni mimi hapa.” Akamwambia: “Chukua ukatoe swadaqah.” Akasema: “Hivi kuna ambaye ni fakiri kuliko mimi, ee Mtume wa Allaah? Ninaapa kwa Allaah hakuna kati ya milima miwili hii watu wa nyumba ambao ni mafukara kuliko watu wa nyumbani kwangu.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akacheka mpaka yakaonekana magego yake. Kisha akasema: “Walishe watu wa nyumbani kwako.”[1]
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
”Jimaa kwa upande wa mwenye kufunga ina mfanano na hedhi na kupiga chuku kwa upande wa kuwa ni utoaji wa kitu mwilini, na ina mfanano na kula na kunywa kwa upande wa matamanio.”
Akaendelea kusema:
”Jimaa kwa kuwa ni sababu ya kutoka kwa manii ambapo inachukua hukumu ya kutapika, hedhi na kuumikwa, kwa kuwa ni aina ya utoaji wa kitu mwilini. Kwa upande wa kuwa ni moja ya matamanio mawili, imepewa hukumu kama ya kula na kunywa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesimulia kutoka kwa Mola Wake kwamba amesema kuhusu mfungaji:
”Ameacha chakula chake na kinywaji chake kwa ajili Yake.”[2]
Kwa hivyo mtu kuacha kile anachokitamani kwa ajili ya Allaah ni ´ibaadah iliyokusudiwa ambayo mtu analipwa thawabu kwayo.”
Jimaa ni miongoni mwa neema kubwa zaidi za mwili na ni furaha ya nafsi na upanuzi wake. Huchochea matamanio, damu na mwili zaidi kuliko kula. Ikiwa shaytwaan hupita ndani ya mwanadamu kama damu inavyopita na chakula huipanua damu na hivyo nafsi ikaelekea zaidi kwenye matamanio, basi maana hii katika jimaa ni kubwa zaidi. Kwa sababu jimaa huupanua zaidi mwelekeo wa nafsi kuelekea matamanio na huushughulisha moyo mbali na ´ibaadah. Bali jimaa ndiyo kilele cha matamanio na matamanio yake ni makubwa zaidi kuliko matamanio ya chakula na kinywaji. Ndiyo maana aliyefanya jimaa alilazimishwa kutoa kafara sawa na ya ambaye kamfananisha mke wake na mama yake; nayo ni kumuacha huru mtumwa au kile kinachosimama nafasi yake kwa Sunnah na kwa maafikiano ya wanazuoni, kwa sababu jambo hili ni zito zaidi na visababishi vyake vina nguvu zaidi na uharibifu wake ni mkubwa zaidi. Hii ndio hekima kubwa zaidi kati ya hekima mbili za kuharamishwa jimaa. Ama kwa upande wa kuudhoofisha mwili kama ilivyo katika utoaji wa kitu mwilini, hiyo ni hekima nyingine. Kwa hivyo jimaa ikawa inafanana na kutapika na hedhi na katika hilo ni kali zaidi kuliko mambo hayo mawili. Ndiyo
[1] al-Bukhaariy (1936) na Muslim (1111).
[2] al-Bukhaariy (1894), (1904) na Muslim (1151).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 38-39
- Imechapishwa: 10/03/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 38-39
Imechapishwa: 10/03/2026
https://firqatunnajia.com/39-jimaa-inamfunguza-mfungaji/