387. Je, inafaa kwa mtu kusema kuwa maiti amehamia katika rehema za Allaah?

Swali: Ni ipi hukumu ya kusema kwamba maiti ni mwenye kurehemewa, amefunikwa na rehema za Allaah (تغمده الله برحمته), au amehamia katika rehema za Allaah (انتقل إلى رحمة الله)?

Jibu: Hapana vibaya kusema kwamba fulani ni mwenye kurehemewa au kwamba amefunikwa na rehema za Allaah. Kwa sababu kusema kwao hivo ni kwa njia ya kudhania vyema na kuwa na matarajio na sio kwa njia ya kuelezea. Vivyo hivyo “Amehamia katika rehema za Allaah”.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/452)
  • Imechapishwa: 29/05/2026