22 – Kutia mwanya kwenye meno

Miongoni mwa makosa yanayokiuka Shari´ah ni kutengeneza mwanya kwa lengo la kupendeza na kujipamba. Hayo yanafanyika kwa kule kuyachonga kwa kutumia kinoleo mpaka kujitokeze kati ya meno uwazi madogo. Hata hivyo ikiwa meno yana matatizo kama kutoboka au muonekano mbaya na hivyo yanahitaji matibabu au marekebisho kwa sababu za kiafya, basi kufanya hivyo ni halali kwa kuwa ni sehemu ya tiba.

  • Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 33
  • Imechapishwa: 20/03/2026