36- Bibiharusi anaweza kuwahudumia wanaume
Hapana ubaya bibiharusi mwenyewe akawahudumia wageni midhali atakuwa amejisitiri[1] na kukaaminiwa kutotokea fitina kutokana na Hadiyth ya Sahl bin Sa´d aliyesema:
“Wakati Abu Usayd as-Sa´di alipooa na kumwingilia mkewe alimwalika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pamoja na Maswahabah zake. Hakuna aliyewatengenezea chakula wala kuwahudumia nacho isipokuwa mkewe Umm Usayd.” Katika upokezi mwingine imekuja ya kwamba aliroweka tende kwenye chombo cha udongo usiku uliopita. Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomaliza kula, alimpakulia na kuwapa. Kwa hivyo mkewe siku hiyo akawa ndiye mwenye kuwahudumia ilihali yeye ndiye alikuwa bibiharusi.”[2]
[1] Namaanisha kujistiri ambako kumewekwa katika Shari´ah. Kumeshurutishwa juu yake masharti manane:
1- Kufunika mwili mzima isipokuwa uso na vtanga vya mikono.
2- Nguo isiwe yenye mapambo.
3- Iwe nzito na isiwe yenye kuonyesha.
4- Isionyeshe kitu kwenye mwili wake kutokana na kubana kwake.
5- Isiwe ni yenye kutiwa manukato.
6- Lisifanane na mavazi ya wanaume.
7- Lisifanane na mavazi ya makafiri.
8- Lisiwe ni vazi la kutaka umaarufu/kutaka kuonekana.
Tumetunga kitabu maalum kinachobainisha dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah juu ya kusihi kwa masharti haya. Kimechapishwa katika maktabaha “as-Salafiyyah” huko Cairo mwaka wa 1374 kwa anwani: “Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah fiyl-Kitaab was-Sunnah”. Kisha maktabah “al-Islaamiyyah” ikachapisha chapa nyingi. Mara ya mwisho niliwapa idhini maktabah “al-Islaamiyyah” ya kuchapisha iliyoko Oman.
[2] Ameipokea al-Bukhaariy (09/200), (205) na (206) katika “Aadaab-ul-Mufrad” (746), Muslim (06/103), Abu ´Awaanah katika “as-Swahiyh” yake (01/131/8-2), Ibn Maajah (590-591) na wengineo.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 177-178
- Imechapishwa: 27/03/2018

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 177-178
Imechapishwa: 27/03/2018
https://firqatunnajia.com/38-hapana-ubaya-bibiharusi-kuwahudumia-wageni/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)