38. Hapa ndipo kutadhihiri ubora wa mfungaji

Uamuzi wa mwisho katika suala hili ni kwamba pale ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoeleza kwamba harufu hiyo nzuri itakuwa siku ya Qiyaamah, basi ni kwa sababu huo ndio wakati ambapo hujitokeza malipo ya matendo na yale yanayolazimishwa nayo katika kheri na shari, basi hujitokeza kwa viumbe harufu nzuri ya hicho kinachotoka kwenye kinywa cha aliyefunga ikilinganishwa na harufu ya miski, kama ambavyo hujitokeza ndani yake harufu ya damu ya aliejeruhiwa katika njia Yake ikilinganishwa na harufu ya miski, kama ambavyo hujitokeza ndani yake mambo ya siri na kuonekana juu ya nyuso na huwa waziwazi na hujitokeza ndani yake ubaya wa harufu ya makafiri na weusi wa nyuso zao. Pale ambapo alieleza kwamba hapo ni wakati wa kutoka harufu mbaya na wakati wa jioni, basi ni kwa sababu huo ndio wakati wa kujitokeza athari ya ´ibaadah. Aidha huwa wakati huo harufu nzuri ya hilo kwa harufu ya miski kwa upande wa Allaah (Ta´ala) na kwa upande wa Malaika Wake. Ingawa harufu hiyo ni yenye kuchukiwa na viumbe, basi huenda kitu kinachochukiwa kwa watu kikawa kinachopendeza kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na kinyume chake. Hakika watu huichukia kwa sababu inapingana na maumbile yao na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) huipenda na huiangalia vizuri kwa sababu inapatana na amri Yake, ridhaa Yake na mapenzi Yake. Ndio maana huwa Kwake huwa bora zaidi kuliko harufu ya miski kwetu sisi. Basi pale itakapokuwa siku ya Qiyaamah itadhihiri harufu hiyo nzuri kwa viumbe na huwa waziwazi. Vivyo hivyo inapokuja katika athari zote za matendo ya kheri na ya shari. Hakika kukamilika kwa kujitokeza kwake na kuwa waziwazi kunapatikana huko Aakhirah. Huenda matendo yakawa na nguvu na ikaongezeka mpaka ikalazimu kujitokeza kwa baadhi ya athari yake juu ya mja katika dunia – ni mamoja jambo la kheri na la shari – kama inavyoonekana kwa macho na kwa muono wa ndani. Ibn ´Abbaas amesema:

”Hakika ya tendo jema lina mwangaza katika uso, nuru moyoni, nguvu katika mwili, upana katika rizki na upendo katika nyoyo za viumbe. Hakika ya tendo ovu lina weusi katika uso, giza moyoni, udhaifu katika mwili, upungufu katika rizki na chuki katika nyoyo za viumbe.”

´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Mja hatendi tendo lolote isipokuwa Allaah shuka Yake ya juu; ikiwa ni kheri basi ni kheri na ikiwa ni shari basi ni shari.”[1]

Hili ni jambo linalojulikana ambalo wanashirikiana ndani yake wenye muono wa ndani na wengineo, mpaka inafikia kwamba mtu mzuri mwema hutambuliwa kwa harufu nzuri hata kama hajapaka manukato. Hivyo hujitokeza harufu nzuri ya roho yake juu ya mwili wake na nguo zake. Fasiki ni kinyume chake. Mwenye mafua ambaye ameathirika na hewa, hufikia kutonusa wala hii wala ile, bali mafua yake humpelekea kuzikataa. Hii basi ndiyo hukumu ya mwisho katika suala hili – na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye anayejua zaidi yaliyo sahihi.

[1] Ahmad katika “az-Zuhd” (157), Ibn-ul-Mubaarak katika “az-Zuhd” (17) na Abu Daawuud katika “az-Zuhd” (111-112).

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 66-68
  • Imechapishwa: 10/08/2025