Tambueni kwamba mwenye kufunga yuko katika ´ibaadah kubwa sana na haifai kwake kuharibu usafi wake kutokana na maneno au matendo yasiyofaa yanayoharibu ´ibaadah hiyo. Kwa kuwa yuko katika ´ibaadah muda wote wa funga yake, hata anapolala ikiwa amekusudia kwa usingizi huo kujipa nguvu kwa ajili ya swawm na swalah ya usiku, basi katika hali hiyo usingizi wake huo huhesabiwa kuwa ni ´ibaadah. Kwa hivyo haimpasi ajitie katika hali isiyoendana na ´ibaadah hii. Ndiyo maana Salaf walipokuwa wakifunga wakikaa misikitini na wakisema:
”Tunaihifadhi swawm yetu na hatumsengenyi mtu yeyote.”
Wakifanya hivo kwa jitihada zao za kuilinda swawm yao.
Kwa hiyo muislamu mwenye kufunga si lazima awe msikitini muda wote, kwa sababu anahitaji kufanya kazi na shughuli za maisha yake. Lakini ni wajibu kwake ahifadhi heshima ya swawm yake popote alipo. Ni haramu kwake kutamka maneno mabaya kama matusi na laana, hata kama mtu atamtukana au atamlaani hairuhusiwi kumrudishia kwa mfano wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Ikiwa ni siku ya swawm ya mmoja wenu, basi asiseme maneno machafu wala asitende ujinga. Ikiwa mtu atapigana naye au atamtukana, basi aseme: ”Mimi ni mwenye kufunga.”[1]
al-Haakim na al-Bayhaqiy wamepokea kutoka kwake:
”Swawm si kuacha chakula na kinywaji tu, bali swawm ni kuacha maneno yasiyo na maana na maneno machafu. Ikiwa mtu atakutukana au akakufanyia ujinga, basi sema: ”Mimi ni mwenye kufunga.”[2]
[1] al-Bukhaariy (1894) na Muslim (1151).
[2] al-Haakim (01/431), al-Bayhaqiy (04/270) na al-Daylamiy (5224). al-Haakim amesema:
”Swahiyh juu ya masharti ya Muslim na hawakuipokea.”
na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 35-36
- Imechapishwa: 09/03/2026
Tambueni kwamba mwenye kufunga yuko katika ´ibaadah kubwa sana na haifai kwake kuharibu usafi wake kutokana na maneno au matendo yasiyofaa yanayoharibu ´ibaadah hiyo. Kwa kuwa yuko katika ´ibaadah muda wote wa funga yake, hata anapolala ikiwa amekusudia kwa usingizi huo kujipa nguvu kwa ajili ya swawm na swalah ya usiku, basi katika hali hiyo usingizi wake huo huhesabiwa kuwa ni ´ibaadah. Kwa hivyo haimpasi ajitie katika hali isiyoendana na ´ibaadah hii. Ndiyo maana Salaf walipokuwa wakifunga wakikaa misikitini na wakisema:
”Tunaihifadhi swawm yetu na hatumsengenyi mtu yeyote.”
Wakifanya hivo kwa jitihada zao za kuilinda swawm yao.
Kwa hiyo muislamu mwenye kufunga si lazima awe msikitini muda wote, kwa sababu anahitaji kufanya kazi na shughuli za maisha yake. Lakini ni wajibu kwake ahifadhi heshima ya swawm yake popote alipo. Ni haramu kwake kutamka maneno mabaya kama matusi na laana, hata kama mtu atamtukana au atamlaani hairuhusiwi kumrudishia kwa mfano wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Ikiwa ni siku ya swawm ya mmoja wenu, basi asiseme maneno machafu wala asitende ujinga. Ikiwa mtu atapigana naye au atamtukana, basi aseme: ”Mimi ni mwenye kufunga.”[1]
al-Haakim na al-Bayhaqiy wamepokea kutoka kwake:
”Swawm si kuacha chakula na kinywaji tu, bali swawm ni kuacha maneno yasiyo na maana na maneno machafu. Ikiwa mtu atakutukana au akakufanyia ujinga, basi sema: ”Mimi ni mwenye kufunga.”[2]
[1] al-Bukhaariy (1894) na Muslim (1151).
[2] al-Haakim (01/431), al-Bayhaqiy (04/270) na al-Daylamiy (5224). al-Haakim amesema:
”Swahiyh juu ya masharti ya Muslim na hawakuipokea.”
na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 35-36
Imechapishwa: 09/03/2026
https://firqatunnajia.com/37-maana-halisi-ya-swawm-2/