Imekuja pia kwamba kusengenya kunamfunguza mfungaji. Imaam Ahmad amepokea katika ”Musnad” yake:
”Kuna wanawake wawili waliokuwa wamefunga katika zama za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao wakakaribia kufa kwa kiu. Jambo hilo lilipomfikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akawaapuuza. Kisha akatajiwa nao tena ambapo akawaita na akawaamuru watapike yale yaliyomo matumboni mwao. Wakatoa matapishi yaliyojaa kikombe, yakiwa ni usaha, damu, majimaji ya damu na nyama mbichi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Hakika wawili hawa wamefunga dhidi ya yale Allaah aliyoyahalalisha kwao na wakafungua kwa yale Allaah aliyoyaharamisha juu yao. Mmoja wao alikaa kwa mwenzake wakawa wanakula nyama za watu.”[1]
Yaliyotokea kwa wanawake hao ni katika miujiza aliyoifanya Allaah kupitia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili iwabainikie watu athari mbaya na chafu za kusengeny usengenyi. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا ۚ أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا
”Wala wasisengenyane baadhi yenu wengine. Je, anapenda mmoja wenu kwamba ale nyama ya nduguye aliyekufa?”[2]
Hadiyth hii inajulisha ya kwamba kusengenya kunamfunguza mfungaji. Ufunguzi huu ni wa kimaana. Maana yake ni kubatilika kwa thawabu kwa mtazamo wa kikosi kikubwa cha wanazuoni.
[1] Ahmad (05/431).
[2] 79:12
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 35
- Imechapishwa: 07/03/2026
Imekuja pia kwamba kusengenya kunamfunguza mfungaji. Imaam Ahmad amepokea katika ”Musnad” yake:
”Kuna wanawake wawili waliokuwa wamefunga katika zama za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao wakakaribia kufa kwa kiu. Jambo hilo lilipomfikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akawaapuuza. Kisha akatajiwa nao tena ambapo akawaita na akawaamuru watapike yale yaliyomo matumboni mwao. Wakatoa matapishi yaliyojaa kikombe, yakiwa ni usaha, damu, majimaji ya damu na nyama mbichi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Hakika wawili hawa wamefunga dhidi ya yale Allaah aliyoyahalalisha kwao na wakafungua kwa yale Allaah aliyoyaharamisha juu yao. Mmoja wao alikaa kwa mwenzake wakawa wanakula nyama za watu.”[1]
Yaliyotokea kwa wanawake hao ni katika miujiza aliyoifanya Allaah kupitia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili iwabainikie watu athari mbaya na chafu za kusengeny usengenyi. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَلَا يَغْتَب بَّعْضُكُم بَعْضًا ۚ أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ أَن يَأْكُلَ لَحْمَ أَخِيهِ مَيْتًا
”Wala wasisengenyane baadhi yenu wengine. Je, anapenda mmoja wenu kwamba ale nyama ya nduguye aliyekufa?”[2]
Hadiyth hii inajulisha ya kwamba kusengenya kunamfunguza mfungaji. Ufunguzi huu ni wa kimaana. Maana yake ni kubatilika kwa thawabu kwa mtazamo wa kikosi kikubwa cha wanazuoni.
[1] Ahmad (05/431).
[2] 79:12
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 35
Imechapishwa: 07/03/2026
https://firqatunnajia.com/36-swawm-na-kuwasengenya-watu/