34. Jawabu kwa watu wa batili kwa jumla na kwa kina

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mlango wa saba

Jawabu kwa watu wa batili kwa jumla na kwa kina

Nitakutajia kitu katika yale aliyotaja Allaah katika Kitabu Chake jibu kwa maneno ambayo washirikina wa zama zetu wanatumia kama hoja dhidi yetu.

MAELEZO

Halafu mtunzi (Rahimahu Allaah) anataja kuwa katika kitabu chake hichi atataja kila hoja wanayotumia washirikina dhidi ya Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah). Atafichua hoja tata hizi ambazo kwa hakika sio hoja. Bali ni hoja tata tu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 55
  • Imechapishwa: 11/11/2023