Kuna makundi mawili yaliyopotea katika siku hii:
1 – Waliojifananisha na mayahudi kwa kuifanya ´Aashuuraa’ kuwa msimu wa shangwe na furaha kwa namna ya kwamba wanaonyesha alama za furaha kama kupaka hinaa, kuweka wanja, kuwatunzia familia matumizi ya ziada, kupika vyakula vya anasa n.k. Hawa ni miongoni mwa wajinga waliojibu batili kwa batili na Bid´ah kwa Bid´ah.
2 – Waliyoifanya ´Aashuuraa’ kuwa siku ya huzuni, maombolezo na vilio kwa sababu ya kuuawa kwa al-Husayn bin ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa).
Hivyo wakaonyesha alama za kipindi kabla ya kuja Uislamu kama kujipiga mashavu, kurarua nguo, kuimba mashairi ya huzuni na kusimulia khabari nyingi za uongo. Lengo ni kufungua mlango wa fitina na kugawa ummah. Hili ni tendo la waliopotea juhudi zao katika dunia huku wakidhani wanafanya jambo zuri.
Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amewaongoza Ahl-us-Sunnah kufanya alilowaamrisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kufunga na huku wakizingatia kutowaiga mayahudi na wakaepuka yale aliyowaamrisha shaytwaan katika Bid´ah. Hivyo basi, sifa zote njema na shukrani ni za Allaah.
- Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 60-61
- Imechapishwa: 20/05/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)