34. Dalili ya swalah na swawm na tafsiri ya Tawhiyd

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya swalah na zakaah na tafsiri ya Tawhiyd, ni Kauli Yake (Ta´ala):

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ

“Hawakuamrishwa jengine isipokuwa wamuabudu Allaah pekee hali ya kumtakasia yeye dini, wenye kupondoka kwenye haki na kuiacha batili, na wasimamishe swalah na watoe  zakaah – na hiyo ndio dini iliyosimama imara – na hiyo ndiyo dini iliyosimama imara.” (al-Bayyinah 98:05)

MAELEZO

Dalili ya swalah na zakaah na tafsiri ya Tawhiyd ni maneno Yake (Ta´ala):

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ

“Hawakuamrishwa jengine isipokuwa wamuabudu Allaah pekee hali ya kumtakasia yeye dini, wenye kupondoka kwenye haki na kuiacha batili, na wasimamishe swalah na watoe  zakaah – na hiyo ndio dini iliyosimama imara  – na hiyo ndiyo Dini iliyosimama imara.” (98:05)

Ndio tafsiri ya Tawhiyd:

وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ

“… na wasimamishe swalah na watoe zakaah – na hiyo ndiyo dini iliyosimama imara.” (98:05)

Allaah (Ta´ala) amesema vilevile:

فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَخَلُّوا سَبِيلَهُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

“Lakini wakitubu na wakasimamisha swalah na wakatoa zakaah, basi waacheni huru – hakika Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (09:05)

بَرَاءَةٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ إِلَى الَّذِينَ عَاهَدتُّم مِّنَ الْمُشْرِكِينَ

”Huku ni kujitoa Allaah na Mtume Wake dhimma kwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa washirikina.” (09:01)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 15/01/2017