Kuhusu wafananishaji Qur-aan imewaraddi. Allaah (Ta´ala) amesema:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye.” (42:11)
وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ
“Na wala hakuna yeyote anayefanana na kulingana Naye.” (112:04)
هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا
“Je, unamjua mwengine anaye jina kama Lake?” (19:65)
فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ
“Basi msimfanyie Allaah wenza na hali ya kuwa nyinyi mnajua.” (02:22)
Mwenza ni anayeshabihiana na kufanana Naye. Amekataza kumfanyia Allaah anaoshabihiana na kufanana Naye kutoka katika viumbe Wake (Subhaanahu wa Ta´ala). Hakuna kitu kinachofanana Naye.
Hii ndio ´Aqiydah ya Jahmiyyah katika suala la mikono miwili ya Allaah (´Azza wa Jall). Wanaraddiwa namna hii vile walivyopindisha. Ndio ´Aqiydah vilevile ya wafananishaji na wakanushaji na wanaraddiwa kupitia maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 93
- Imechapishwa: 09/01/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)