33. Mlango kuhusu maneno Yake (Ta´ala) “Kwa Allaah pekee tegemeeni ikiwa nyinyi ni waumini!”

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

1- Allaah (Ta´ala) amesema:

وَعَلَى اللَّـهِ فَتَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ

“Kwa Allaah pekee tegemeeni ikiwa nyinyi ni waumini!” (al-Maaidah 05:23)

2-

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ

”Hakika waumini ni wale ambao anapotajwa Allaah nyoyo zao zinajaa khofu, na wanaposomewa Aayah Zake huwazidishia imani na kwa Mola wao wanategemea.” (al-Anfaal 08:02)

3-

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ حَسْبُكَ اللَّـهُ وَمَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ

”Ee Nabii! Anakutoshele za Allaah na anayekufuata miongoni wa waumini.” (al-Anfaal 08:64)

4-

وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُ

“Na yeyote yule atakayemtegemea Allaah, basi Yeye humtosheleza.” (at-Twalaaq 65:03)

5- Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

حَسْبُنَا اللّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ

“Allaah pekee anatutosheleza na Yeye ndiye mbora wa kutegemewa.”

neno hili lilisemwa na Ibraahiym (´alayhis-Salaam) alipotupwa ndani ya moto na alilisema Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati alipoambiwa:

الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُواْ لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَاناً

”Wale ambao waliambiwa na watu: “Hakika watu wamekusanyika dhidi yenu hivyo basi waogopeni”; yakawazidishia imani… “[1] (Aal ´Imraan 03:173)

Ameipokea al-Bukhaariy na an-Nasaa´iy.

MAELEZO

1- Allaah (Ta´ala) amesema:

وَعَلَى اللَّـهِ فَتَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ

“Kwa Allaah pekee tegemeeni ikiwa nyinyi ni waumini!”

Alichokusudia mwandishi (Rahimahu Allaah) kwa mlango huu ni kwamba lililo la wajibu ni kumtegemea Allaah na kuegemea Kwake katika mambo yote ya dini na ya dunia. Kutegemea maana yake ni kumwachia kila kitu Allaah, kumwamini, kuamini kwamba Yeye ndiye anasababisha sababu na kwamba kila kitu kiko mikononi Mwake; kwamba Anachotaka huwa na Asichotaka hakiwi. Aidha anatakiwa kutambua kuwa tayari kumeshapangwa kila kitu na kwamba mja hana uwezo wa chochote anachotaka ikiwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) hakukikadiria. Vilevile kutegemea kunahusiana na mtu kufanya sababu.

 2-

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّـهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ

”Hakika waumini ni wale ambao anapotajwa Allaah nyoyo zao zinajaa khofu, na wanaposomewa Aayah Zake huwazidishia imani na kwa Mola wao wanategemea.”

 3-

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ حَسْبُكَ اللَّـهُ وَمَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ

”Ee Nabii! Anakutoshele za Allaah na anayekufuata miongoni wa waumini.”

4-

وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُ

“Na yeyote yule atakayemtegemea Allaah, basi Yeye humtosheleza.”

Allaah atakutosheleza wewe na wafuasi wako na msiwahitajie wengine. Yule ambaye yuko na Allaah hamuhitajii mwingine. Ni wajibu kwa muumini kumtegemea Allaah pamoja vilevile na kufanya sababu zinazonufaisha duniani na Aakhirah na aziepuke sababu zinazomdhuru duniani na Aakhirah. Anapaswa kufanya matendo mema na kujiepusha na maasi ili aweze kupata Pepo. Anatakiwa kula na kunywa na kujiepusha na yale yote yenye kumdhuru. Kwa sababu haya ni sababu ya [kuendelea] kuishi kwake. Haya hayapingani na kutegemea. Kutegemea kumekusanya mambo mawili:

1- Kumwamini Allaah na kwamba Yey ndiye anayesababisha sababu na anayeyaendesha mambo.

2- Kufanya sababu.

Kutegemea haina maana kwamba mtu aache kufanya sababu, kama wanavosema Suufiyyah. Bali mja anatakiwa kukusanya yote mawili na wakati huohuo amwombe Allaah msaada.

5- Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

حَسْبُنَا اللّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ

“Allaah pekee anatutosheleza na Yeye ndiye mbora wa kutegemewa.”

neno hili lilisemwa na Ibraahiym (´alayhis-Salaam) alipotupwa ndani ya moto na alilisema Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati alipoambiwa:

الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُواْ لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَاناً

”Wale ambao waliambiwa na watu: “Hakika watu wamekusanyika dhidi yenu hivyo basi waogopeni”; yakawazidishia imani… “

Ameipokea al-Bukhaariy na an-Nasaa´iy.

Ibraahiym (´alayhis-Salaam) alisema hivo wakati Namruud alipomtuma ndani ya moto. Allaah akamwokoa kutokamana na moto huo na:

قُلْنَا يَا نَارُ كُونِي بَرْدًا وَسَلَامًا عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ

“Tukasema: “Ee moto! Kuwa baridi na salama kwa Ibraahiym!” (al-Anbiyaa´ 21:69)

Allaah akamlinda kutokamana na shari yake na shari zao na akamwokoa yeye na akawa ni ishara na miujiza inayofahamisha juu ya ukweli wa ujumbe wake. Kadhalika yalisemwa na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati alipoambiwa kwamba washirikika wamekusanyika kwa ajili ya kuwashambulia kwa mara nyingine. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

حَسْبُنَا اللّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ

“Allaah pekee anatutosheleza na Yeye ndiye mbora wa kutegemewa.”

Ndipo Allaah akamlinda.

Hivi ndivyo anvyotakiwa muislamu kusema wakati wa matatizo. Lakini haina maana kwamba asifanye sababu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema hivo na akafanya maandalizi ya vita, akabeba silaha na akavaa kofia maalum kwa ajili ya vita. Vivyo hivyo wakafanya Maswahabah. Wakati wa vita vya Ahzaab walichimba handaki. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا خُذُوا حِذْرَكُمْ فَانفِرُوا ثُبَاتٍ أَوِ انفِرُوا جَمِيعًا

“Enyi mlioamini! Shikeni hadhari yenu; tokeni makundi moja moja au tokeni kwa pamoja.” (an-Nisaa´ 04:71)

[1] al-Bukhaariy (4563).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 111-112
  • Imechapishwa: 23/10/2018