Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:
16 – Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya chuku ilihali ni Muhrim na akafanya chuku ilihali amefunga.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy.
17 – Shaddaad bin Aws (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwendea bwana mmoja al-Baqiy´ ilihali anafanya chuku katika Ramadhaan ambapo akasema: “Amefungua mwenye kuumika na mwenye kuumikwa.”[2]
Wameipokea watano isipokuwa at-Tirmidhiy. Ameisahihisha Ahmad, Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan.
18 – Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Mwanzoni wakati ilikuwa inachukizwa kufanya chuku kwa mfungaji Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpitia Ja´far bin Abiy Twaalib aliyekuwa anafanya chuku ilihali amefunga ambapo akasema: “Wawili wote hawa wamefungua.”[3]
Kisha baadaye Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamruhusu mfungaji kuumikwa. Anas mwenyewe alikuwa akiumikwa ilihali amefunga.
Ameipokea ad-Daaraqutwniy ambaye ameona kuwa ni yenye nguvu.
MAELEZO
Hadiyth ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ni dalili ya kufaa mfungaji kupiga chuku na kwamba haiharibu swawm, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipiga chuku akiwa amefunga. Haya ndio maoni ya kikosi kikubwa cha wanazuoni, wakiwemo wale maimamu watatu; Abu Haniyfah, Maalik na ash-Shaafi’iy. Pia ndio chaguo dhahiri la al-Bukhaariy na ndio maoni yaliyotiliwa nguvu na Ibn Hazm[4]. Dalili inayounga mkono hilo ni yale yaliyotangulia kupitia kwa ´Abdur-Rahmaan bin Abiy Laylaa ambaye amesema kwamba mtu mmoja miongoni mwa Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuumikwa na kuunganisha swawm, lakini hakuwaharamishia Maswahabah zake kufanya hivo….[5] Pia al-Bukhaariy amepokea kwa cheni yake ya wapokezi kupitia kwa Shu´bah ambaye ameeleza kuwa amemsikia Thaabit al-Bunaaniy akieleza kuwa Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) aliulizwa: ”Je, mliona kuumikwa kwa mfungaji kuwa ni jambo lisilopendeza?” – Imekuja katika upokezi mwingine: ”Wakati wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?” Akajibu: ”Hapana, isipokuwa kutokana na unyonge.”[6]
[1] al-Bukhaariy (1938).
[2] Ahmad (2/122), Abu Daawuud (2369), an-Nasaa’iy (3126), Ibn Maajah (1681) na Ibn Hibbaan (3533).
[3] ad-Daaraqutwniy (2260).
[4] al-Muhallaa (06/204-205), “Badai’us-Swanaa´iy’” (02/107), “Bidaayat-ul-Mujtahid” (02/154), “al-Majmuu’” (06/349).
[5] as-Sunan (2374) na mlolongo wa wapokezi wake ni Swahiyh.
[6] Swahiyh-ul-Bukhaariy (1940).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/42-44)
- Imechapishwa: 19/02/2025

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/42-44)
Imechapishwa: 19/02/2025
https://firqatunnajia.com/33-hadiyth-mtume-alifanya-chuku-ilihali-ni-muhrim/