Amesema tena kuwa amemsikia Sufyaan ath-Thawriy akisema:

”Wanayachafua mavazi yao kisha wanawaamrisha watu waje kuyaosha.”

138 – Abu Sa´iyd Muhammad bin Muusa as-Swayrafiy ametukhabarisha: Abul-´Abbaas Muhammad bin Ya´quub al-Aswamm ametuhadithia: ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal ametuhadithia: ´Ubaydullaah bin ´Umar al-Qawaariyriy ametuhadithia: Yahyaa bin Sa´iyd amesema:

”Hakuna kitu ninachokikhofia kwa Sufyaan isipokuwa mapenzi yake juu ya Hadiyth.”

139 – Muhammad bin Ahmad bin Rizq ametukhabarisha: Ismaa´iyl bin ´Aliy al-Khutwamiy, Abu ´Aliy bin as-Swawwaaf na Ahmad bin Ja´far bin Hamdaan wametuzindua: ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal ametukhabarisha: Baba yangu amenihadithia: Abu Qatwan ametukhabarisha: Nimemsikia Ibn ´Awn akisema:

”Natamani isingelikuwa upande wangu wala dhidi yangu.”

 Bi maana elimu.

140 – Abu Qatwan amesimulia kwamba Shu´bah amesema:

”Hakuna kitu nilichokishikilia ambacho nachelea kisiniingize Motoni kama Hadiyth.”

141 – Abu Ishaaq Ibraahiym bin ´Umar bin Ahmad al-Barmakiy ametukhabarisha: Muhammad bin ´Abdillaah bin Khalaf bin Bakhiyt ad-Daqqaaq ametukhabarisha: ´Umar bin Muhammad al-Jawhariy ametukhabarisha: Abu Bakr al-Athram ametukhabarisha: Nimemsikia Abu ´Abdillaah Ahmad bin Hanbal akitaja masimulizi ya Shu´bah na akasema maneno mfano wa:

”Unajua kwamba alikuwa ni mkweli katika matendo.”

142 – Abu Nu´aym al-Haafidhw amenikhabarisha kwa kunipa ijaza: Habiyb bin al-Hasan na Ahmad bin Ibraahiym al-´Attwaar wametuhadithia: Sahl bin Abiy Sahl ametuhadithia: Bishr bin Khaalid ametuhadithia: Shabaabah ametuhadithia:

”Niliingia kwa Shu´bah katika ile siku aliyokufa ndani yake. Alikuwa akilia. Nikasema: ”Ni kwa kukata tamaa huku, ee Abu Bistwaam? Pata bishara njema, kwa sababu una nafasi nzuri katika Uislamu.” Akasema: ”Niache. Natamani laiti ningekuwa mafuta kwenye sauna na sikujua Hadiyth.”

143 – Ahmad bin Muhammad bin Ahmad al-´Atiyqiy amenikhabarisha: Muhammad bin al-´Abbaas al-Khazzaaz ametuhadithia: Ja´far bin Muhammad as-Swandaliy ametuhadithia: Muhammad bin Haaruun Abu Nashiytw al-Harbiy ametuhadithia:

”Nilikutana na Bishr bin al-Haarith njiani ambapo akanikataza Hadiyth na wanafunzi wake. Nikakutana pia na Yahyaa bin Sa´iyd al-Qattwaan, ambaye nimefikiwa na khabari kuwa amesema: ”Hakika mimi nampenda kijana huyu na namchukia.” Alipoulizwa sababu akasema: ”Nampenda kutokana na ´Aqiydah yake na namchukia kwa sababu ya kutafuta kwake Hadiyth.”

144 – Abul-´Abbaas al-Fadhwl bin ´Abdir-Rahmaan bin al-Fadhwl al-Abhariy ametukhabarisha: Abu Bakr bin al-Muqriy ametuhadithia huko Aswbahaan: Ahmad bin Shu´ayb al-Antwaakiy ametuhadithia: Muhammad bin Ya´quub ad-Daynawariy ametuhadithia: al-´Abbaas bin ´Abdil-´Adhwiym ametuhadithia: Bishr bin al-Haarith amesema:

”Ukitaka kunufaika kwa Hadiyth, basi usijifunze nazo nyingi na wala usiketi na wale wanaozitafuta.”

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 85-88
  • Imechapishwa: 22/05/2024
  • Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy