Imepokelewa kutoka kwa Maaswahabah wakuu (Radhiya Allaahu ´anhum) na waliokuja baada yao kuhusu kufaa kupangusa juu ya soksi hata kama ni nyembamba. Imaam an-Nawawiy amesema katika maelezo yake ya ”al-al-Muhadhdhab”:
”Wenzetu – Shaafi´iyyah – wamenukuu kutoka kwa ´Umar na ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kuhusu kufaa kupaka juu ya soksi hata kama ni nyembamba. Wamenukuu pia kutoka kwa Abu Yuusuf, Muhammad, Ishaaq na Daawuud.”
Kisha an-Nawawiy akasema:
”Waliolihalalisha hilo, hata kama ni nyepesi, wamejengea hoja kwa Hadiyth ya al-Mughiyrah kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipangusa juu ya soksi na viatu vyake. Kumepokelewa kutoka kwa Abu Muusa mfano wa hilo kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”
Ndani yake kuna nyongeza juu ya yaliyotangulia, nayo ni tamko la wazi la kujuzu kutoka kwao hata kama ni nyepesi, ingawa hilo linaweza kufahamika pia kutokana na upokezi uliokuja kwa ujumla kabla, kwa kuwa asili katika tamko la ujumla ni kubaki juu ya ujumla wake mpaka ije dalili ya kulifunga, kama ambavyo tamko la kijumla hubaki na hukumu yake mpaka litolewe ushahidi wa kulibainisha. Ubainifu wa hilo utakuja kutokana na yale aliyoyasema Imaam Ibn Hazm (Rahimahu Allaah).
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 55
- Imechapishwa: 13/04/2026
Imepokelewa kutoka kwa Maaswahabah wakuu (Radhiya Allaahu ´anhum) na waliokuja baada yao kuhusu kufaa kupangusa juu ya soksi hata kama ni nyembamba. Imaam an-Nawawiy amesema katika maelezo yake ya ”al-al-Muhadhdhab”:
”Wenzetu – Shaafi´iyyah – wamenukuu kutoka kwa ´Umar na ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kuhusu kufaa kupaka juu ya soksi hata kama ni nyembamba. Wamenukuu pia kutoka kwa Abu Yuusuf, Muhammad, Ishaaq na Daawuud.”
Kisha an-Nawawiy akasema:
”Waliolihalalisha hilo, hata kama ni nyepesi, wamejengea hoja kwa Hadiyth ya al-Mughiyrah kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipangusa juu ya soksi na viatu vyake. Kumepokelewa kutoka kwa Abu Muusa mfano wa hilo kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”
Ndani yake kuna nyongeza juu ya yaliyotangulia, nayo ni tamko la wazi la kujuzu kutoka kwao hata kama ni nyepesi, ingawa hilo linaweza kufahamika pia kutokana na upokezi uliokuja kwa ujumla kabla, kwa kuwa asili katika tamko la ujumla ni kubaki juu ya ujumla wake mpaka ije dalili ya kulifunga, kama ambavyo tamko la kijumla hubaki na hukumu yake mpaka litolewe ushahidi wa kulibainisha. Ubainifu wa hilo utakuja kutokana na yale aliyoyasema Imaam Ibn Hazm (Rahimahu Allaah).
Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 55
Imechapishwa: 13/04/2026
https://firqatunnajia.com/32-kupangusa-juu-ya-soksi-nyembamba/