32. Jambo ambalo walinganizi wanapaswa kulitilia mkazo

Kushikamana na Qur-aan na Sunnah ni jambo la lazima. Kwa hivyo ni lazima kwa walinganizi wanaolingania kwa Allaah kuyatilia hayo umuhimu mkubwa na wayaweka mbele ya macho yao.

Wako walinganizi ambao wanayatanguliza mbele matamanivu na maoni yao mbele ya Qur-aan na Sunnah ijapo anaita matamanivu na maoni haya jina jingine kwa ajili ya kutaka kutakasa kwenda kwake kinyume. Hakika majina haya hayana faida wala maana yoyote. Majina hayo hayanufaishi chochote mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa sababu majina hayabadilishi uhalisia wa mambo.

Wale ambao wanafanya manufaa ya Da´wah kupingana na Qur-aan na Sunnah na hivyo wakayatanguliza mbele ya dalili za Qur-aan na Sunnah, hakika watu hawa wamepotea mbali na njia ilionyooka. Miongoni mwa mambo wanayoyafanya ni kwamba yule anayepingana nao na akafichua ile batili wanayoificha basi wanajuzisha kumzulia uongo na kumrushia tuhuma. Kwa sababu wanaona kuwa mambo hayo ni kwa manufaa ya Da´wah. Hawajali maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا

“Wale wanaowaudhi waumini wa kiume na waumini wa kike pasi na wao kufanya kosa lolote, basi kwa hakika wamejibebea uzushi mkuu wa dhuluma na dhambi ya wazi.”[1]

Hawazingatii Aayah hii kwa sababu wanaona kuwa wanatakiwa kutanguliza mbele ya manufaa ya Da´wah, jambo ambalo ni kosa kabisa na upotevu wa wazi. Ni lazima kwa yule mwenye kujivika tabia hii atubu kwa Allaah (´Azza wa Jall) na ajirejee. Hayo mambo anayoyafanya ni upotevu wa wazi na kosa ovu. Hayo ndio mambo ambayo Salaf wametahadharisha. Uhakika wa mambo ni kwamba tabia hii wameichukua kutoka kwa Ahl-ur-Ray´ na wakaachana nao. Kulikuwa na vita vikubwa baina yao. Mwishowe Allaah akawanusuru Ahl-us-Sunnah dhidi yao na akaitokomeza batili yao. Himdi, fadhilah na neema zinarudi kwa Allaah.

[1] 33:58

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 76-78
  • Imechapishwa: 17/11/2020