al-Qummiy amesema wakati alipokuwa anafasiri:

وَإِذِ ابْتَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ رَبُّهُ بِكَلِمَاتٍ فَأَتَمَّهُنَّ ۖ قَالَ إِنِّي جَاعِلُكَ لِلنَّاسِ إِمَامًا ۖ قَالَ وَمِن ذُرِّيَّتِي ۖ قَالَ لَا يَنَالُ عَهْدِي الظَّالِمِينَ

“Na [kumbuka] Alipojaribiwa Ibraahiym na Mola wake kwa maneno [maamrisho], naye akayatimiza. [Allaah] Akasema: “Hakika Mimi Nakufanya uwe kiongozi [mfano] kwa watu.” [Ibraahiym] Akasema: “Na katika kizazi change?” Akasema: “Haiwafikii ahadi Yangu madhalimu.” (02:124)

“Inahusiana na jinsi Allaah Alivyomjaribu wakati alipoota ndotoni kuwa atamchinga mwanae. Ibraahiym akatimiza maamrisho na alikuwa ni mwenye azima. Wakati alipokuwa mwenye azima na kufanya yale Aliyomwamrisha Allaah ndipo Allaah akawa Amesema:

إِنِّي جَاعِلُكَ لِلنَّاسِ

“Hakika Mimi Nakufanya uwe kiongozi [mfano] kwa watu.”

Ibraahiym akasema:

وَمِن ذُرِّيَّتِي

“Na kizazi changu?”

لَا يَنَالُ عَهْدِي الظَّالِمِينَ

“Haiwafikii ahadi Yangu madhalimu.”

Bi maana ahadi Yangu haimfikii kiongozi yeyote dhalimu.”[1]

Anawakusudia Makhaliyfah watatu na wale wenye kupita kwenye nyayo zao.

Mkaguzi wa kitabu ametaja taaliki ya Hujjat-ul-Islaam al-Jazaairiy:

“Kwenye Tafsiyr ya Qur-aan ya Imaam al-´Askariy kumepokelewa maana ya maamrisho kutoka kwa as-Swaadiyq na kwamba ni yale maneno ambayo Aadam alimwambia Mola Wake na hivyo Akamsamehe, nayo ni:

“Ee Allaah! Ninakuomba kwa haki ya Muhammad, ´Aliy, Faatwimah, al-Hasan na al-Husayn unisamehe.”

Kukasemwa: “Ee mjukuu wa Mtume wa Allaah! Ni nini maana ya:

فَأَتَمَّهُنَّ

“… naye akayatimiza.”

Akasema: “Akamtimizia nayo al-Qaa´im[2].”

Mashaa Allaah! Yale ambayo al-Qummiy ameghafilika nayo anayafidia huyu Hujjat-ul-Islaam na yaliyo na ukhurafi wa al-Qaa´im. Je, Mitume katika wakati wa Aadam walikuwa wanaamini ´Aqiydah ya Raafidhwah ilio na ukhurafi wa al-Qaa´im? Je, Qur-aan imeteremshwa na ´Aqiydah hii? Je, watu wa nyumba ya kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni bora kuliko Ibraahiym (´alayhis-Salaam) mpaka atawassul kupitia wao? Je, unaweza kweli kupata uongo ulio mbaya zaidi juu ya Allaah na juu ya Mitume Wake kuliko huu hapa? Kutawassul kupitia watu ni Bid´ah inayopelekea kwenye shirki. Ni kitu ambacho Allaah Amemtakasa nacho Aadam, Ibraahiym na Mitume wengine wote.

Kauli yake “Akamtimizia nayo al-Qaa´im” ni msemo wa kipumbavu. Allaah Alimjaribu Ibraahiym (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) kwa Shari´ah, Tawhiyd, maamrisho na makatazo. Akayatimiza kwa njia nzuri kabisa itakikanayo. Hivyo ndio Allaah Akamlipa na kumsifu. Allaah (Ta´ala) Amesem:

وَإِبْرَاهِيمَ الَّذِي وَفَّىٰ

“Na Ibraahiym aliyetimiza [ahadi].” (53:37)

Tunaomba kinga kwa Allaah kutokamana na upotoshaji na uongo wa Raafidhwah. Je, Ibraahiym aliyaelekeza maamrisho ya Allaah ya ´Aqiydah na Shari´ah kwa al-Qaa´im ambaye alikuwa hata hajapatikana? Kutokana na uzushi huu maana yake ni kwamba Ibraahiym alikwepa jukumu Alilobebeshwa na Allaah na akampasia nalo al-Qaa´im wa uongo. Je, huku si kumtukana vibaya Ibraahiym? Ndio. Haya na mfano wake yanawaonyesha wale walio na busara jinsi Raafidhwah hawa masikini walivo na Uislamu na dini yao imejengwa juu ya uongo, mchezo na upotoshaji wa dini ya Allaah.

[1] Tafsiyr al-Qummiy (1/59).

[2] al-Mahdiy

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 67
  • Imechapishwa: 19/03/2017