131 – Abu Twaalib Muhammad bin al-Fath al-Harbiy ametukhabarisha: ´Umar bin Ahmad al-Waa-idhw ametukhabarisha: Abu Habiyb al-´Abbaas bin Ahmad al-Bartiy ametukhabarisha: Sawwaar bin ´Abdillaah ametuhadithia: Nimemsikia Ibn ´Uyaynah akisema:
”Ningeulizwa ni kwa nini nazitafuta Hadiyth, basi nisingelijua nini cha kujibu.”
132 – Abu Muhammad bin ´Abdillaah bin Yahyaa bin ´Abdil-Jabbaar as-Sukkariy amenikhabarisha: Muhammad bin ´Abdillaah bin Ibraahiym ash-Shaafi´iy ametukhabarisha: Ja´far bin Muhammad bin al-Azhar ametukhabarisha: al-Ghalaabiy ametukhabarisha:
”Bwana mmoja alimuuliza Ibn ´Uyaynah juu ya cheni ya wapokezi ya Hadiyth, ambapo akajibu: ”Utafanya nini na cheni ya wapokezi? Kuhusu wewe, umekwishafikiwa na hekima yake na yamekulazimu mazingatio yake.”
133 – ´Abdul-´Aziyz bin ´Aliy al-Azjiy ametukhabarisha: ´Umar bin Muhammad bin Ibraahiym al-Bajaliy ametukhabarisha: Ahmad bin ´Ubaydillaah bin ´Ammaar ath-Thaqafiy ametukhabarisha: Abu Zayd ´Umar bin Shabbah ametukhabarisha: Khallaad bin Yaziyd al-Arqatw amenihadithia:
”Nilimwendea Sufyaan bin ´Uyaynah, ambapo akasema: ”Hakuna kitachokujilia isipokuwa tu ujinga, na si utafutaji elimu. Lau majirani zako wangelitosheka na elimu yako basi ingeliwatosha.” Kisha akakusanya rundo la changarawe, akaligawanya kwa kidole chake na kusema: ”Hii ni elimu. Umechukua nusu yake na sasa umekuja kutafuta nusu iliobaki. Ukiulizwa kama kweli umefanyia kazi ile nusu ya kwanza na ukawa mkweli, basi utajibu na kusema hapana. Ndipo utaulizwa ni kwa nini unajizidishia mzigo juu ya mzigo. Yafanyie kazi yale uliyojifunza mwanzo.”
134 – ´Aliy bin Abiy ´Aliy al-Mu-addil amenikhabarisha: Ahmad bin Yuusuf al-Azraq bin Ya´quub bin Ishaaq al-Buhluul at-Tannuukhiy ametuhadithia: Baba yangu ametukhabarisha: Abu Bakr Ahmad bin Mansuur ar-Ramaadiy ametuhadithia: Nu´aym – yaani Ibn Hammaad – amenihadithia:
”Nilimuuliza Ibn ´Uyaynah – au kuna mtu mwingine aliyemuuliza: ”Ni nani mwanachuoni?” Akasema: ”Ni yule anayeipa kila Hadiyth haki yake.”
135 – Abul-Qaasim al-Hasan bin al-Hasan bin ´Aliy bin al-Mundhir al-Qaadhwiy ametukhabarisha: Ismaa´iyl bin Muhammad as-Swaffaar ametukhabarisha: Muhammad bin Ishaaq Abu Bakr ametuhadithia: ´Ubaydullaah bin Muusa ametukhabarisha: Sufyaan ath-Thawriy amesema:
”Natamani kama kamwe ningekuwa sikutafuta Hadiyth na mikono yangu isingelikuwa imekatwa kuanzia hapa bali kuanzia hapa.” Akaashiria mwanzo wa kwenye kiganja cha mkono kisha akaashiria begani. Akasema: ”Hapana, bali kuanzia hapa.”
136 – Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy bin ´Abdillaah at-Twabariy amenikhabarisha: Muhammad bin Bakraan al-Bazzaaz ametuzindua: Abu ´Abdillaah bin Makhlad al-´Attwaar ametuhadithia: Muhammad bin ´Umar bin al-Hakam ametukhabarisha: Ishaaq bin Ibraahiym ametukhabarisha: Hajjaaj bin Muhammad ametukhabarisha: Sufyaan ath-Thawriy amesema:
”Watu wameridhika kwa Hadiyth na wakaacha matendo.”
137 – Muhammad bin ´Abdillaah bin Abaan al-Hiytiy ametukhabarisha: Ahmad bin Salmaan an-Najjaad ametuhadithia: Muhammad bin ´Abduus ametukhabarisha: Ahmad bin ´Abdis-Swamad ametukhabarisha: Nimemsikia Shu´ayb bin Harb akisema:
”Nimemsikia Sufyaan baada ya kupata ujumbe: ”Yafanyieni kazi mwanzo yale mliyojifunza. Kisha baadaye nijilieni ili nipate kuwasimulia Hadiyth.”
- Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy al-Khatwiyb al-Baghdaadiy (afk. 463)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Iqtidhwaa’-ul-´Ilm al-´Amal, uk. 83-85
- Imechapishwa: 22/05/2024
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)