Hali kadhalika inatakiwa kusema juu ya sifa zingine ya kwamba huruma, radhi, ghadhabu, uwezo, mkono na mguu vyote vinajulikana. Kuhusu namna yake haijulikani. Hatujui namna ya huruma Yake ilivyo, ghadhabu Zake, mkono Wake, mguu Wake na macho Yake vyote hatujui namna vilivyo na wala hatupekui. Bali tunazithibitisha na kuzipitisha kama vilivyokuja. Tunasema kuwa Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona, tunasema kuwa ni Mwenye mikono miwili kama alivyosema (Ta´ala):
وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللَّـهِ مَغْلُولَةٌ ۚ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُوا بِمَا قَالُوا ۘ بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ
“Mayahudi wakasema: “Mkono wa Allaah imefumbwa”. Mikono yao ndio iliyofumbwa na wamelaaniwa kwa yale waliyoyasema. Bali mikono Yake imekunjuliwa hutoa atakavyo.” (05:64)
Vilevile imekuja katika Hadiyth Swahiyh inayosema:
“Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) ataweka mguu Wake juu ya Moto kisha pawe sawa. Hapo ndio utasema “Inatosha! Inatosha!”[1]
Vilevile Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ameeleza kuwa anamghadhibikia yule mwenye kumuasi na humridhia yule mwenye kumtii. Anawarehemu waja Wake. Zote hizi ni katika sifa Zake (Jalla wa ´Alaa):
“Allaah anawacheka watu wawili ambapo mmoja wao kamuua mwenzake. Halafu wote wawili wanaingia Peponi.”[2]
Kughadhibika Kwake, kuridhia Kwake, kusikia Kwake, kuona Kwake na sifa zake zingine zote zinalingana na Yeye peke yake na wala hashabihiani na viumbe Vyake kwa chochote katika hayo kutokana na kanuni isemayo:
لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (42:11)
Ahlus-Sunnah wal-Jamaa´ah wanathibitisha Aayah na Hadiyth zinazozungumzia sifa, uthibitishaji ambao hamna ndani yake ufananishaji na wakati huohuo wanamtakasa Allaah (Jalla wa ´Alaa) kufanana na viumbe Wake utakaso usiokuwa ndani yake na ukanushaji. Inahusiana na ukanushaji ulioambatana na uthibitishaji.
[1] al-Bukhaariy (4848) na Muslim (2846).
[2] al-Bukhaariy (2826) na Muslim (1890).
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 43
- Imechapishwa: 22/10/2024

Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 43
Imechapishwa: 22/10/2024
https://firqatunnajia.com/31-namna-hii-ndivo-ahl-us-sunnah-al-jamaaah-wanathibitisha-sifa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)