15 – Mwanamke kupanda peke yake na dereva asiye Mahram

Miongoni mwa makosa yanayoenda kinyume na Shari´ah ni mwanamke kupanda peke yake na dereva asiyekuwa Mahram. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanaume yeyote asikae peke yake na mwanamke isipokuwa akiwa na Mahram wake.”

Ameipokea al-Bukhaariy.

Bali hali hii ni khatari zaidi kuliko chemba nyingi, kwa sababu dereva ana gari mkononi mwake na anaweza kuiendesha anapotaka.

  • Muhusika: Dr. ´Abdul-´Aziyz bin Daawuud al-Faaiz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tawjiyhaat wa Tanbiyhaat lil-Fataati al-Muslimah, uk. 30
  • Imechapishwa: 03/03/2026