2- Dhuhr
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa katika zile Rak´ah mbili za mwanzo akisoma al-Faatihah na Suurah nyingine. Akirefusha zaidi katika Rak´ah ya kwanza kuliko anavyofanya katika hiyo ya pili[1].
Wakati mwingine alikuwa anaweza kuirefusha Rak´ah ya kwanza sana kiasi cha kwamba pindi swalah inapoanzwa mtu alikuwa anaweza kwenda makaburini al-Baqiy´, akifanya haja yake, anarudi nyumbani kwake, anatawadha na halafu anafika msikitini ilihali Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) bado yuko katika ile Rak´ah ya kwanza[2].
Walikuwa wakifikiri kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anarefusha hivo ili watu waweze kuiwahi hiyo Rak´ah ya kwanza[3].
Katika kila Rak´ah alikuwa akisoma kiasi cha sawa na Aayah thelathini kama Suurah “as-Sajdah” kukiwemo al-Faatihah[4].
Mara nyingine akisoma (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Suurah “at-Twaariq”, “al-Buruuj”, “al-Layl” na mfano wa Suurah mfano wake[5].
Huenda wakati mwingine akisoma (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Suurah “al-Inshiqaaq” na mfano wake[6].
Walikuwa wakitambua kuwa Dhuhr na ´Aswr anasoma kwa kutikisika kwa ndevu zake[7].
[1] al-Bukhaariy na Muslim.
[2] Muslim na al-Bukhaariy katika ”Juz’-ul-Qiraa-ah”.
[3] Abu Daawuud kwa mlolongo wa wapokezi mzuri na Ibn Khuzaymah (1/165/1).
[4] Ahmad na Muslim.
[5] Abu Daawuud na at-Tirmidhiy ambaye ameisahihisha na hali kadhalika Ibn Khuzaymah (2/62/1).
[6] Ibn Khuzaymah katika ”as-Swahiyh” (2/67/1).
[7] al-Bukhaariy na Abu Daawuud.
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 98-99
- Imechapishwa: 06/02/2017
2- Dhuhr
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa katika zile Rak´ah mbili za mwanzo akisoma al-Faatihah na Suurah nyingine. Akirefusha zaidi katika Rak´ah ya kwanza kuliko anavyofanya katika hiyo ya pili[1].
Wakati mwingine alikuwa anaweza kuirefusha Rak´ah ya kwanza sana kiasi cha kwamba pindi swalah inapoanzwa mtu alikuwa anaweza kwenda makaburini al-Baqiy´, akifanya haja yake, anarudi nyumbani kwake, anatawadha na halafu anafika msikitini ilihali Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) bado yuko katika ile Rak´ah ya kwanza[2].
Walikuwa wakifikiri kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anarefusha hivo ili watu waweze kuiwahi hiyo Rak´ah ya kwanza[3].
Katika kila Rak´ah alikuwa akisoma kiasi cha sawa na Aayah thelathini kama Suurah “as-Sajdah” kukiwemo al-Faatihah[4].
Mara nyingine akisoma (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Suurah “at-Twaariq”, “al-Buruuj”, “al-Layl” na mfano wa Suurah mfano wake[5].
Huenda wakati mwingine akisoma (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Suurah “al-Inshiqaaq” na mfano wake[6].
Walikuwa wakitambua kuwa Dhuhr na ´Aswr anasoma kwa kutikisika kwa ndevu zake[7].
[1] al-Bukhaariy na Muslim.
[2] Muslim na al-Bukhaariy katika ”Juz’-ul-Qiraa-ah”.
[3] Abu Daawuud kwa mlolongo wa wapokezi mzuri na Ibn Khuzaymah (1/165/1).
[4] Ahmad na Muslim.
[5] Abu Daawuud na at-Tirmidhiy ambaye ameisahihisha na hali kadhalika Ibn Khuzaymah (2/62/1).
[6] Ibn Khuzaymah katika ”as-Swahiyh” (2/67/1).
[7] al-Bukhaariy na Abu Daawuud.
Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 98-99
Imechapishwa: 06/02/2017
https://firqatunnajia.com/31-kisomo-katika-dhuhr/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)