211 – Abu ´Abdillaah bin Budjayr na Abu Khaythamah amenihadithia: Ibn ´Ulayyah ametuhadithia, kutoka kwa Yuunus, kutoka kwa al-Hasan, kutoka kwa ´Utayy, kutoka kwa Ubayy bin Ka´b, aliyesema:
”Hakika chakula cha mwanaadamu kimepigwa mfano kwa dunia, hata akikitia viungo na kukitia chumvi. Hakika mwisho wake unajulikana na kila mtu.”
Kwa maana ya mbegu, haijalishi kitu atakitia chumvi kiasi gani.
212 – Ishaaq bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia, kutoka kwa Ibn-ul-Murtafiy´, aliyeeleza kuwa amemsikia Ibn-uz-Zubayr akisema kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):
وَفِي أَنفُسِكُمْ ۚ أَفَلَا تُبْصِرُونَ
”… na katika nafsi zenu, je, hamuoni?”[1]
”Kwa maana njia ya choo na mkojo.”
213 – Muhammad bin ´Abbaad ametuhadithia: Ghassaan bin Maalik ametuhadithia, kutoka kwa Hammaad bin Salamah, kutoka kwa al-Kalbiy, kutoka kwa Abu Swaalih, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye amesema kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):
فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ إِلَىٰ طَعَامِهِ
”Basi atazame mtu chakula chake.”[2]
”Kwa maana kwenye kinyesi chake.”
214 – Baba yangu amenihadithia: Rawh bin ´Ubaadah ametukhabarisha: Sa´iyd bin ´Ubayd al-Jubayriy ametukhabarisha, kutoka kwa Bakr bin ´Abdillaah al-Muzaniy, ambaye ameeleza kuwa bwana mmoja amemukhabarisha:
”Alisuhubiana Ka´b al-Ahbaar kwa miaka kumi na moja. Alipokaribia kufa akasema: ”Mimi nimesuhubiana nawe kwa miaka kumi na moja nikitaka kukuuliza kuhusu jambo lakini nilikuwa nakuogopa.” Akasema: ”Uliza unachotaka.” Akasema: ”Niambie ni kwa nini mwanaadamu anaposimama baada ya kufanya kwake haja, hurudisha macho yake na kuitazama?” Akasema: ”Naapa kwa Yule ambaye nafsi ya Ka´b ipo mikononi Mwake! Hakika umeniuliza kuhusu jambo ambalo Allaah (´Azza wa Jall) ameliteremsha ndani ya Tawraat kwa Muusa: ”Angalia dunia yako unayoikusanya!”
215 – Abu Ja´far Muhammad bin Abiy Rajaa’ al-Qurashiy amenihadithia: Muhammad bin Kunaasah al-Asdiy ametuhadithia:
Kila kitu ulichotiya chumvi katika ladha ya dunia
na kukipamba juu ya meza
Kitakuwa baada ya kukila rangi
lakini ni miongoni mwa rangi mbaya zaidi
Na pindi muda wa kukitoa mwilini unapowadia,
basi fikiria juu ya unyonge wa mwanaadamu
Na unapoekiweka mahali,
basi geuka na uzingatie mahali hapo
216 – Ahmad bin Jamiyl ametuhadithia: ´Abdullaah ametukhabarisha: Ma´mar ametukhabarisha, kutoka kwa Zayd bin Aslam, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Kuwa mbali na kiburi ni kukaa pamoja na waumini mafukara.”
217 – ´Aliy bin al-Ja´d ametuhadithia: Sufyaan bin Sa´iyd ametukhabarisha, kutoka kwa Habiyb bin Abiy Thaabit, kutoka kwa Yahyaa bin Ja´dah, ambaye amesema:
”Yule atakayeweka uso wake kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall) hali ya kusujudu basi amejiepusha mbali na kiburi.”
[1] 51:21
[2] 80:24
- Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 258-262
- Imechapishwa: 26/03/2026

Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 258-262
Imechapishwa: 26/03/2026
https://firqatunnajia.com/31-izingatie-dunia-unayojikusanyia/