Masimulizi yote haya yamepokelewa na ´Abdur-Razzaaq katika “al-Muswannaf” (745, 773, 779, 781 na 782), Ibn Abiy Shaybah katika “al-Muswannaf” (1/188) na al-Bayhaqiy (1/285). Nyingi katika cheni za wapokezi wake ni Swahiyh kutoka kwao. Baadhi yao zina zaidi ya njia moja ya upokezi. Moja katika hizo ni njia ya Qataadah kutoka kwa Anas kwamba alikuwa akipaka juu ya soksi kama akivyopaka juu ya soksi za ngozi. Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh. Ameipokea ´Abdur-Razzaaq (779) na iko pia kwa Ibn Abiy Shaybah (1/188) kwa ufupi. Kwa wote wawili kupitia njia ya Yahyaa al-Bakkaa´, ambaye ameeleza ya kwamba amemsikia Ibn ´Umar akisema:
”Kupaka juu ya soksi ni kama kupaka juu ya soksi za ngozi.”
Naafiy´ akapokea hilo kutoka kwake na akasema:
”Hizo ziko katika daraja ya soksi za ngozi.”
Ameipokea Ibn Abiy Shaybah kwa cheni ya wapokezi nzuri kutoka kwake.
Vivyo hivyo amepokea kutoka kwa Ibraahiym an-Nakha´iy kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kutoka kwake.
Kwa hiyo baada ya kuthibiti kupaka juu ya soksi za ngozi kutoka kwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum), je, si tuna haki ya kusema juu ya yule mwenye kupuuza ambaye Ibraahiym amesema kuhusiana na kupangusa juu ya soksi za ngozi:
“Basi mwenye kuacha hilo kwa kulipuuza, basi hakika hilo ni kutoka kwa shaytwaan.”?
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 54
- Imechapishwa: 13/04/2026
Masimulizi yote haya yamepokelewa na ´Abdur-Razzaaq katika “al-Muswannaf” (745, 773, 779, 781 na 782), Ibn Abiy Shaybah katika “al-Muswannaf” (1/188) na al-Bayhaqiy (1/285). Nyingi katika cheni za wapokezi wake ni Swahiyh kutoka kwao. Baadhi yao zina zaidi ya njia moja ya upokezi. Moja katika hizo ni njia ya Qataadah kutoka kwa Anas kwamba alikuwa akipaka juu ya soksi kama akivyopaka juu ya soksi za ngozi. Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh. Ameipokea ´Abdur-Razzaaq (779) na iko pia kwa Ibn Abiy Shaybah (1/188) kwa ufupi. Kwa wote wawili kupitia njia ya Yahyaa al-Bakkaa´, ambaye ameeleza ya kwamba amemsikia Ibn ´Umar akisema:
”Kupaka juu ya soksi ni kama kupaka juu ya soksi za ngozi.”
Naafiy´ akapokea hilo kutoka kwake na akasema:
”Hizo ziko katika daraja ya soksi za ngozi.”
Ameipokea Ibn Abiy Shaybah kwa cheni ya wapokezi nzuri kutoka kwake.
Vivyo hivyo amepokea kutoka kwa Ibraahiym an-Nakha´iy kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kutoka kwake.
Kwa hiyo baada ya kuthibiti kupaka juu ya soksi za ngozi kutoka kwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum), je, si tuna haki ya kusema juu ya yule mwenye kupuuza ambaye Ibraahiym amesema kuhusiana na kupangusa juu ya soksi za ngozi:
“Basi mwenye kuacha hilo kwa kulipuuza, basi hakika hilo ni kutoka kwa shaytwaan.”?
Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 54
Imechapishwa: 13/04/2026
https://firqatunnajia.com/31-haijuzu-kupuuza-kupangusa-juu-ya-soksi/