204 – Muhammad bin al-Husayn na Muhammad bin Yahyaa bin Abiy Haatim wamenihadithia: ´Abdus-Swamad bin ´Abdil-Waarith ametuhadithia: Haashim al-Kuufiy ametuhadithia: Zayd al-Khath´amiy amenihadithia, kutoka kwa Asmaa’ bint ´Umays al-Khath´amiyyah, ambaye amesimulia kuwa amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
”Ni mbaya mno mja ambaye amejivuna na kupitiliza na kumsahau Jabari Aliyetukuka. Na ni mbaya mno mja ambaye amejiona na kujifaharisha na kumsahau Mkubwa Mwenye Kunyanyuka. Na ni mbaya mno mja ambaye amepuuzia na kuzembea na kusahau makaburi na kuoza. Na ni mbaya mno mja ambaye amekithiri dhuluma na kupitiliza na kusahau mwanzo na mwisho.”[1]
205 – Abu ´Abdir-Rahmaan ´Abdullaah bin Abiy Ziyaad ametuhadithia: Sayyaar ametuhadithia, kutoka kwa Ja´far bin Sulaymaan, kutoka kwa Thaabit, aliyesimulia:
”Nimefikiwa na khabari kwamba kulisemwa: ”Ee Mtume wa Allaah, ni ukubwa uliyoje wa kiburi cha fulani!” Akasema: ”Je, si baada yake kuna mauti?”
206 – Abu Khaythamah ametuhadithia: Wahb bin Jariyr ametuhadithia: Nimemsikia as-Saq´ab bin Zuhayr akisimulia kutoka kwa Zayd bin Aslam, kutoka kwa ´Atwaa’ bin Yasaar, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr, ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika Nuuh alipokaribia kufa, aliwaita wanawe wawili na akasema: ”Hakika mimi nawaachia usia, ninakuamrisheni mambo mawili na ninakukatazeni mambo mawili. Ninawakatazeni shirki na kiburi, na ninakuamrisheni ”Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah”. Hakika mbingu, ardhi na vilivyomo ndani yao lau vingewekwa katika upande wa mizani na ikawekwa ”Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah” katika upande wa pili, ingelikuwa nzito zaidi kuliko hivyo. Na lau mbingu, ardhi na vilivyomo ndani yao vingelikuwa ni pete na ”Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah” ikawekwa juu yake basi ingelivivunja. Na ninakuamrisheni kusema:
سبحان الله وبحمده
”Allaah ametakasika kutokana na mapungufu na himdi zote njema anastahiki Allaah.”
Kwani hiyo ni swalah ya kila kitu na kwa hizo kila kitu kinaruzukiwa.”[2]
207 – ´Abdur-Rahmaan bin Swaalih ametuhadithia: al-Muhaaribiy ametuhadithia, kutoka kwa Yuusuf as-Sabbaagh, kutoka kwa al-Hasan, aliyesema:
”Atakayeshona viatu vyake, kutia kiraka nguo yake na kuupiga uso wake kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall), basi amejiepusha na kiburi.”
208 – Surayj bin Yuunus ametuhadithia: Yahyaa bin Abiy Bukayr ametuhadithia: Sulaymaan bin al-Mughiyrah ametuhadithia kwamba ´Iysaa bin Maryam (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Twubaa kwa yule ambaye Allaah (´Azza wa Jall) amemfundisha Kitabu Chake kisha hakufa hali ya kuwa na kiburi.”
209 – Ahmad bin ´Abdil-A´laa ash-Shaybaaniy ametuhadithia: Abu Muhammad al-Baswriy ametuhadithia: al-Hasan amesema:
”Ajabu kwa mwanaadamu anaosha mkono wake kutokana na kinyesi mara mbili kisha anafanya kiburi. Anapingana na Allaah (´Azza wa Jall), Jabari wa mbingu na ardhi!”
210 – Khaalid bin Khidaash ametuhadithia: Hammaad bin Zayd ametuhadithia, kutoka kwa ´Aliy bin Zayd, kutoka kwa al-Hasan, kutoka kwa adh-Dhwahhaak bin Sufyaan al-Kilaabiy, ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Ee Dwahhaak, chakula chako ni kipi?” Akasema: ”Nyama na maziwa.” Akasema: ”Mwishowe kinakuwa nini?” Akasema: ”Kile ambacho umejua.” Akasema: ”Hakika Allaah (´Azza wa Jall) amepiga mfano wa kinachotoka kwa mwanaadamu kwa dunia.”[3]
[1] at-Tirmidhiy (2448), ambaye amesema kuwa ni ngeni. Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (2448).
[2] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “as-Swahiyhah” (134).
[3] Ahmad (3/452). Tazama ”as-Swahiyhah” (382) ya al-Albaaniy.
- Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 253-257
- Imechapishwa: 26/03/2026

Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 253-257
Imechapishwa: 26/03/2026
https://firqatunnajia.com/30-nyasia-wa-mwisho-wa-nuuh/