6- Mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya kutengeneza katika jamii:
Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaona kuwa jamii ya Kiislamu kutengamaa kwake hakuwezi kukamilika isipokuwa mpaka ifuate Shari´ah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa ajili hiyo ndio maana wanaona kuamrisha mema na kukataza maovu.
Mema ni kila kile kilichotambuliwa na kukubaliwa na Shari´ah.
Maovu ni kila kile kilichokataliwa na kuharamishwa na Shari´ah.
Wanaona kuwa jamii ya Kiislamu haiwezi kutengamaa isipokuwa kwa uamrishwaji wa mema na ukatazwaji wa maovu. Kutapokosekana jambo hili basi kutatokea mfarakano, kama yanavyoashiria maneno ya Allaah (´Azza wa Jall):
وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفلِحُونَ وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ تَفَرَّقُوا وَاخْتَلَفُوا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ
Wawepo kutoka kwenu watu wanaolingania kheri na kuamrisha mema na unaokataza maovu – hao ndio waliofaulu. Na wala msiwe kama wale waliofarikiana na wakakhitilafiana baada ya kuwajia hoja ya wazi – na hao watapata adhabu kuu.”[1]
Jambo hili hii leo limepotea au limekaribia kupotea. Ni mara chache mno utapata mtu anayeamrisha mema na anakataza maovu. Watu watapoacha kazi hii na ikawa kila mmoja anafanya akitakacho basi watu watafarikiana. Lakini wakiamrishana mema na wakakatazana maovu watakuwa Ummah mmoja.
[1] 03:104-105
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy-´Aqiydah wal-´Amal, uk. 41-42
- Imechapishwa: 22/08/2019
6- Mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya kutengeneza katika jamii:
Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaona kuwa jamii ya Kiislamu kutengamaa kwake hakuwezi kukamilika isipokuwa mpaka ifuate Shari´ah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa ajili hiyo ndio maana wanaona kuamrisha mema na kukataza maovu.
Mema ni kila kile kilichotambuliwa na kukubaliwa na Shari´ah.
Maovu ni kila kile kilichokataliwa na kuharamishwa na Shari´ah.
Wanaona kuwa jamii ya Kiislamu haiwezi kutengamaa isipokuwa kwa uamrishwaji wa mema na ukatazwaji wa maovu. Kutapokosekana jambo hili basi kutatokea mfarakano, kama yanavyoashiria maneno ya Allaah (´Azza wa Jall):
وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفلِحُونَ وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ تَفَرَّقُوا وَاخْتَلَفُوا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ
Wawepo kutoka kwenu watu wanaolingania kheri na kuamrisha mema na unaokataza maovu – hao ndio waliofaulu. Na wala msiwe kama wale waliofarikiana na wakakhitilafiana baada ya kuwajia hoja ya wazi – na hao watapata adhabu kuu.”[1]
Jambo hili hii leo limepotea au limekaribia kupotea. Ni mara chache mno utapata mtu anayeamrisha mema na anakataza maovu. Watu watapoacha kazi hii na ikawa kila mmoja anafanya akitakacho basi watu watafarikiana. Lakini wakiamrishana mema na wakakatazana maovu watakuwa Ummah mmoja.
[1] 03:104-105
Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy-´Aqiydah wal-´Amal, uk. 41-42
Imechapishwa: 22/08/2019
https://firqatunnajia.com/30-mfumo-wa-ahl-us-sunnah-katika-kuamrisha-mema-na-kukataza-maovu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)