Ibn Hazm amesimulia katika ”al-Muhallaa” baadhi ya wale tuliyowataja kupangusa juu ya soksi na akasema:
”Kupangusa juu ya kila kinachovaliwa miguuni – miongoni mwa vinavyohalalika kuvaliwa na vinavyofika juu ya vifundo[1] – ni Sunnah, ni mamoja iwe ni soksi za ngozi au soksi za kawaida. Ikiwa kimevaliwa wakati wa wudhuu´, basi inajuzu kupangusa juu yake kwa mkazi mchana mmoja na usiku wake, na kwa msafiri michana mitatu pamoja na nyusiku zake. Kisha haijuzu tena kupangusa.”
Baada ya kusimulia Hadiyth za kupangusa juu ya soksi amesema:
”Miongoni mwa waliotoa kauli ya kupangusa juu ya soksi ni kikosi katika Salaf… Ka´b bin ´Abdullaah amesema:
”Nilimwona ´Aliy bin Abi Twaalib akikojoa kisha akapangusa juu ya viatu vyake na soksi zake.”
Abul-Julaas amesema:
”Ibn ´Umar alikuwa akipangusa juu ya soksi na viatu.”
Ismaa´iyl amesimulia kutoka kwa baba yake, ambaye amesema:
”Nilimwona al-Baraa bin ´Aazib akipaka juu ya soksi zake na viatu vyake.”
Ibraahiym bin Hammaam bin al-Haarith amesimulia:
”Abu Mas´uud al-Badriy alikuwa akipaka juu soksi zake na viatu vyake.”
´Aaswim al-Ahwal amesema:
”Nilimwona Anas bin Maalik akipaka juu yas soksi zake.”
Ibn ´Umar amesema:
”´Umar bin al-Khattwaab alikojoa siku ya Ijumaa kisha akatawadha, akapaka juu ya soksi na viatu na akawaswalisha watu swalah ya ijumaa.”
Abu Waa-il amesema:
”Abu Mas´uud alipaka juu ya soksi zake zilizokuwa za nywele.”
Yahyaa al-Bakkaa´ ameeleza kwamba amemsikia Ibn ´Umar akisema:
”Kupaka juu ya soksi za kawiada ni kama kupaka juu ya soksi za ngozi.”
[1] Kusema kwamba zinatakiwa kufika hadi juu ya vifundo sijui dalili juu ya hilo. Isitoshe ni jambo linaenda na maneno yake Ibn Hazm mwenyewe katika “al-Muhallaa” (2/103), kama nitakavyotaja mwishoni mwa kitabu.
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 53-54
- Imechapishwa: 13/04/2026
Ibn Hazm amesimulia katika ”al-Muhallaa” baadhi ya wale tuliyowataja kupangusa juu ya soksi na akasema:
”Kupangusa juu ya kila kinachovaliwa miguuni – miongoni mwa vinavyohalalika kuvaliwa na vinavyofika juu ya vifundo[1] – ni Sunnah, ni mamoja iwe ni soksi za ngozi au soksi za kawaida. Ikiwa kimevaliwa wakati wa wudhuu´, basi inajuzu kupangusa juu yake kwa mkazi mchana mmoja na usiku wake, na kwa msafiri michana mitatu pamoja na nyusiku zake. Kisha haijuzu tena kupangusa.”
Baada ya kusimulia Hadiyth za kupangusa juu ya soksi amesema:
”Miongoni mwa waliotoa kauli ya kupangusa juu ya soksi ni kikosi katika Salaf… Ka´b bin ´Abdullaah amesema:
”Nilimwona ´Aliy bin Abi Twaalib akikojoa kisha akapangusa juu ya viatu vyake na soksi zake.”
Abul-Julaas amesema:
”Ibn ´Umar alikuwa akipangusa juu ya soksi na viatu.”
Ismaa´iyl amesimulia kutoka kwa baba yake, ambaye amesema:
”Nilimwona al-Baraa bin ´Aazib akipaka juu ya soksi zake na viatu vyake.”
Ibraahiym bin Hammaam bin al-Haarith amesimulia:
”Abu Mas´uud al-Badriy alikuwa akipaka juu soksi zake na viatu vyake.”
´Aaswim al-Ahwal amesema:
”Nilimwona Anas bin Maalik akipaka juu yas soksi zake.”
Ibn ´Umar amesema:
”´Umar bin al-Khattwaab alikojoa siku ya Ijumaa kisha akatawadha, akapaka juu ya soksi na viatu na akawaswalisha watu swalah ya ijumaa.”
Abu Waa-il amesema:
”Abu Mas´uud alipaka juu ya soksi zake zilizokuwa za nywele.”
Yahyaa al-Bakkaa´ ameeleza kwamba amemsikia Ibn ´Umar akisema:
”Kupaka juu ya soksi za kawiada ni kama kupaka juu ya soksi za ngozi.”
[1] Kusema kwamba zinatakiwa kufika hadi juu ya vifundo sijui dalili juu ya hilo. Isitoshe ni jambo linaenda na maneno yake Ibn Hazm mwenyewe katika “al-Muhallaa” (2/103), kama nitakavyotaja mwishoni mwa kitabu.
Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 53-54
Imechapishwa: 13/04/2026
https://firqatunnajia.com/30-kupangusa-juu-ya-soksi-za-kawaida-ni-kama-kupangusa-juu-ya-soksi-za-ngozi/