Kisomo chake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Rak´ah mbili za Fajr kilikuwa kifupi sana[1]. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alikuwa akisema:
“Hivi kweli (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesoma ndani yake al-Faatihah?”[2]
Wakati fulani akisoma katika Rak´ah ya kwanza baada ya al-Faatihah:
قُولُوا آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَمَا أُوتِيَ النَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ
“Semeni: “Tumemwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl na Ishaaq na Ya’quub na al-Asbaatw na aliyopewa Muusa na ´Iysaa na waliyopewa Manabii kutoka kwa Mola wao; hatutofautishi baina ya mmoja miongoni mwao nasi Kwake tunajisalimisha.”[3]
na katika Rak´ah ya pili:
قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ
“Sema: “Enyi Ahl-ul-Kitaab! Njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu – kwamba tusiabudu mwengine isipokuwa Allaah pekee na wala tusimshirikishe Yeye na chochote na wala wasijichukulie baadhi yetu wengine kuwa waungu badala ya Allaah.” [Sema] wakikengeuka, basi semeni: “Shuhudieni kwamba sisi tumejisalimisha kwa Allaah.”[4][5]
Ilikuwa pia inaweza kutokea badala yake anasoma:
فَلَمَّا أَحَسَّ عِيسَىٰ مِنْهُمُ الْكُفْرَ قَالَ مَنْ أَنصَارِي إِلَى اللَّـهِ ۖ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ اللَّـهِ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَاشْهَدْ بِأَنَّا مُسْلِمُونَ
“Basi pindi ‘Iysaa alipohisi kutoka kwao ukafiri [kwa kumuamini], alisema: “Nani watanisaidia [kulingania] katika njia ya Allaah? Wakasema wafuasi watiifu: “Sisi ni wasaidizi wa Allaah! Tumemwamini Allaah; na shuhudia ya kwamba sisi tumejisalimisha kwa Allaah!”[6][7]
Wakati mwingine akisoma Suurah “al-Kaafiruun” katika Rak´ah ya kwanza na Suurah “al-Ikhlaasw” katika Rak´ah ya pili[8]. Alikuwa akisema:
“Ni uzuri uliyoje zilivyo Suurah hizi!”[9]
Pindi alipomsikia mwanaume mmoja akisoma Suurah ya kwanza katika Rak´ah ya mwanzo alisema:
“Huyu ni mja aliyemuamini Mola wake.”
Pindi alipomsikia akisoma Suurah ya pili katika Rak´ah ya pili alisema:
“Huyu ni mja amemtambua Mola wake.”[10]
[1] Ahmad kwa mlolongo wa wapokezi mzuri.
[2] al-Bukhaariy na Muslim.
[3] 2:136
[4] 3:64 Muslim na Abu Daawuud.
[5] Muslim, Ibn Khuzaymah na al-Haakim.
[6] 03:52
[7] Muslim na Abu Daawuud.
[8] Muslim na Abu Daawuud.
[9] Ibn Maajah na Ibn Khuzaymah.
[10] at-Twahaawiy, Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” na Ibn Bishraan. Nzuri kwa mujibu wa Haafidhw Ibn Hajar katika ”al-Ahaadiyth al-´Aaliyah” (16).
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 97-98
- Imechapishwa: 06/02/2017

Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 97-98
Imechapishwa: 06/02/2017
https://firqatunnajia.com/30-kisomo-cha-qu-aan-katika-sunnah-ya-fajr/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)