Abu Qataadah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu swawm ya siku ya ´Aashuuraa’ ambapo akajibu:
“Inafuta madhambi ya mwaka uliopita.”
Imekuja katika upokezi mwingine:
“… na swawm ya siku ya ´Aashuuraa’ natarajia kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kuwa itafuta madhambi ya mwaka uliotangulia.”[1]
Ameipokea Muslim.
MAELEZO
Hadiyth hii ni dalili juu ya fadhilah ya kufunga siku ya ´Aashuuraa’, nayo ni siku ya kumi ya mwezi wa Allaah Muharram kwa mujibu wa maoni sahihi na maarufu zaidi miongoni mwa wanazuoni. Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kwamba aliulizwa kuhusu kufunga siku ya ´Aashuuraa’ ambapo akajibu:
“Sikujua kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifunga siku yoyote kwa kutafuta fadhilah yake kuliko siku hii, wala mwezi wowote isipokuwa huu – kwa maana ya Ramadhaan.”[2]
Kuna maafikiano juu yake.
Kwa hiyo inampasa muislamu afunge siku hii na awahimize familia na watoto wake kuifunga ili kunufaika na fadhilah zake na kwa ajili ya kufuata mfano wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Jaabir bin Samurah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiagiza kufunga siku ya ´Aashuuraa’, alikuwa akituhimiza juu yake na alikuwa akitufuatilia juu ya hilo…”[3]
Ameipokea Muslim.
[1] Muslim (1162), (196) na (197).
[2] al-Bukhaari y (2006) na Muslim (1132).
[3] Muslim (1128).
- Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 57-58
- Imechapishwa: 18/05/2025
Abu Qataadah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu swawm ya siku ya ´Aashuuraa’ ambapo akajibu:
“Inafuta madhambi ya mwaka uliopita.”
Imekuja katika upokezi mwingine:
“… na swawm ya siku ya ´Aashuuraa’ natarajia kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kuwa itafuta madhambi ya mwaka uliotangulia.”[1]
Ameipokea Muslim.
MAELEZO
Hadiyth hii ni dalili juu ya fadhilah ya kufunga siku ya ´Aashuuraa’, nayo ni siku ya kumi ya mwezi wa Allaah Muharram kwa mujibu wa maoni sahihi na maarufu zaidi miongoni mwa wanazuoni. Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kwamba aliulizwa kuhusu kufunga siku ya ´Aashuuraa’ ambapo akajibu:
“Sikujua kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifunga siku yoyote kwa kutafuta fadhilah yake kuliko siku hii, wala mwezi wowote isipokuwa huu – kwa maana ya Ramadhaan.”[2]
Kuna maafikiano juu yake.
Kwa hiyo inampasa muislamu afunge siku hii na awahimize familia na watoto wake kuifunga ili kunufaika na fadhilah zake na kwa ajili ya kufuata mfano wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Jaabir bin Samurah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiagiza kufunga siku ya ´Aashuuraa’, alikuwa akituhimiza juu yake na alikuwa akitufuatilia juu ya hilo…”[3]
Ameipokea Muslim.
[1] Muslim (1162), (196) na (197).
[2] al-Bukhaari y (2006) na Muslim (1132).
[3] Muslim (1128).
Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 57-58
Imechapishwa: 18/05/2025
https://firqatunnajia.com/30-hadiyth-inafuta-madhambi-ya-mwaka-uliopita/