Kwa hivyo kusoma masimulizi na maneno ya watu katika kutetea Sunnah, kusimamisha upwekeshaji na kuwaraddi wazushi ni miongoni mwa mambo muhimu kabisa ambayo mwanafunzi anaweza kuyafanya, ili aweze kupambanua kati ya haki na batili, Sunnah na Bid´ah, uongofu na upotofu. Kwa sababu ´Aqiydah ya maimamu hawa ilienda sambamba na yale aliyokuwemo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na Maswahabah zake baada yake. Walikuwa ni wenye kumwigiliza Mtume wao Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), wakifuata mfumo wao, wakifuata nyayo zao, wakizipa kisogo Bid´ah za wenye kupotosha na wakipita juu ya njia iliyonyooka na iliyo wazi. Kila mmoja alikuwa akimsisitiza mwenzie kufanya hivyo na wakirithiana. Lau ungesoma vitabu vyao vyote, kuanzia cha kwanza hadi cha mwisho, kuanzia mwanzo hadi mwisho, licha ya kutofautiana nchi na zama zao na makaazi na mabara yao kuwa mbalimbali, utaona namna ambavyo wote wako katika ´Aqiydah moja. Wanapita juu ya njia moja, pasi na kugeuka wala kupinda kutokana nayo. Mafundisho yao ni mamoja. Nukuu zao ni moja. Huoni kati yao tofauti wala kufarikiana ijapo kidogo. Bali kama ungeliyakusanya maneno yao na nukuu za watangulizi wao, basi ungeona namna ambavyo kana kwamba yanatoka kwenye ulimi na moyo mmoja[1]. Sababu ni hilo ni kwa kuwa wote walishikamana na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na wakajiweka mbali na matamanio na Bid´ah. Kama al-Awzaa´iy (Rahimahu Allaah) alivosema:
”Tunazunguka na Sunnah kule inakoenda.”[2]
Walikuwa namna hii. Wanazunguka na Sunnah inapokuja katika kuthibitisha na kukanusha. Hawathibitishi isipokuwa tu yale yaliyothibitishwa na Qur-aan na Sunnah, wala hawakanushi isipokuwa tu yale yaliyokanushwa na Qur-aan na Sunnah. Hawaivuki Qur-aan na Hadiyth.
Maimamu hawa hawakuacha kupekua kwa sababu ya kushindwa, udhaifu na kutokuwa na uwezo, bali ni kama alivosema ´Umar bin ´Abdil-Aziyz (Rahimahu Allaah):
“Watangulizi walisimama kwa ujuzi na wakakomeka kwa utambuzi. Walikuwa na nguvu ya kuweza kutafiti, lakini hawakufanya utafiti.”[3]
Yule anayefuata mfumo wa watu basi anakuwa mwenye kufuata njia iliyo salama. Muhammad bin Siyriyn (Rahimahu Allaah) amesema:
“Walikuwa wakisema kwamba mtu kama anashikamana na masimulizi, basi anafuata njia iliyonyooka.”[4]
[1] Tazama “al-Hujjah fiy Bayaan-il-Mahajjah” (2/224-225) ya Abul-Qaasim al-Aswbahaaniy.
[2] al-Laalakaa’iy (1/64).
[3] al-Ibaanah al-Kubraa (1/321) ya Ibn Battwah.
[4] al-Ibaanah al-Kubraa (1/357) ya Ibn Battwah.
- Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 7-9
- Imechapishwa: 26/11/2025

Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 7-9
Imechapishwa: 26/11/2025
https://firqatunnajia.com/3-ili-uweze-kufuata-njia-ilionyooka-iliyo-salama/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket