29. Maswahabah kumi na sita walipangusa juu ya soksi zao za ngozi

Imaam Abu Daawuud amesema:

”´Aliy bin Abiy Twaalib, Abu Mas´uud, al-Baraa’ bin ´Aazib, Anas bin Maalik, Abu Umaamah, Sahl bin Sa´d na ´Amr bin Hariyth walipangusa juu ya soksi. Kitendo hicho kimepokelewa kutoka kwa ´Umar bin al-Khatwtwaab na Ibn ´Abbaas.”[1]

Ibn Sayyid-un-Naas ameongeza katika ”al-Jaamiy” at-Tirmidhiy ´Abdullaah bin ´Umar na Sa´d bin Abiy Waqqaas.”

Katika “Sharh-ul-Iqnaa´” kukaongezwa ´Ammaar na Bilaal[2] na Ibn Abiy Awfaa (Radhiya Allaahu ´anhum). Hivyo jumla ni Maswahabah kumi na nne. Kadhalika al-Mughiyrah na Abu Muusa kwa mapokezi yao mawili yaliyotangulia. Kwa hiyo jumla ikawa Maswahabah kumi na sita.

[1] as-Sunan (159).

[2] Haafidhw Ibn Hadjar amesema katika “Takhriyj Ahaadiyth-il-Muhadhdhab”:

”Kupitia cheni mbili za wapokezi, ambapo moja wapo ni yenye wapokezi wenye kuaminika, ameipokea at-Twabaraaniy kutoka kwa Bilaal.”

  • Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 52
  • Imechapishwa: 13/04/2026