198 – Ishaaq bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Abu Mu´aawiyah ametuhadithia, kutoka kwa ´Umar bin Raashid, kutoka kwa Iyaas bin Salamah al-Akwa´, kutoka kwa baba yake, ambaye ameeeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mtu hatoacha kuiendelea kujikweza mpaka aandikwe miongoni mwa wenye kuburi matokeo yake apatwe na kile kilichowapat katika adhabu.”[1]
199 – Haaruun bin ´Abdillaah amenihadithia: Ibraahiym bin ´Abdir-Rahmaan bin Mahdiy ametuhadithia: Sayyaar ametuhadithia, kutoka kwa Ja´far: Nimemsikia Maalik bin Diynaar akisema:
”Sulaymaan bin Daawuud siku moja aliwaambia ndege, majini, wanadamu na wanyama: ”Watoeni watu 200 000 miongoni mwa wanadamu na 200 0000 miongoni mwa majini.” Akapandishwa juu, mpaka akasikia sauti ya Malaika kwa tasbiyh mbinguni, kisha akashushwa chini mpaka miguu yake ikagusa bahari. Akasikia sauti ikisema: ”Lau ingelikuwa moyoni mwa rafiki yenu kuna uzito wa chembe ya kiburi, ningelimpindua chini zaidi kuliko nilivyompandisha.”
200 – Abu Khaythamah ametuhadithia: Yaziyd bin Haaruun ametuhadithia: Hammaad bin Salamah ametukhabarisha, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas bin Maalik, ambaye ameeleza:
”Abu Bakr alikuwa anatukhutubia na kutaja kuanza kuumbwa kwa mtu mpaka mmoja wetu alikuwa anakereka, na akasema: ”Ametoka katika njia ya mkojo mara mbili.”
201 – Muhammad bin Sallaam al-Jumahiy ametukhabarisha:
”al-Ahnaf bin Qays alikuwa anakaa na Musw´ab bin az-Zubayr juu ya kitanda chake. Siku moja akaja na Musw´ab amenyoosha miguu yake, hakuiweka sawa, na al-Ahnaf akakaa akipeana msongamano fulani. Alipoona jambo hilo akasema: ”Ajabu kwa mwanadamu kujivuna na hali ametoka katika njia ya mkojo mara mbili.”
202 – Ishaaq bin Ibraahiym ametuhadithia: Muslim bin Khaalid ametuhadithia, kutoka kwa Ibn Abiy Najiyh, kutoka kwa Mujaahid, ambaye amesema kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):
وَإِذَا بَطَشْتُم بَطَشْتُمْ جَبَّارِينَ
”Mnapotumia nguvu basi mnatumia nguvu kwa ujabari.”[2]?
”Bi maana kwa upanga.”
203 – Shujaa´ bin al-Ashras ametuhadithia: Yaziyd bin Haaruun ametuhadithia: Hushaym ametukhabarisha, kutoka kwa Ismaa´iyl bin Saalim, kutoka kwa ash-Sha´biy, ambaye amesema:
”Atakayeua watu wawili basi yeye ni mkandamizi.” Kisha akasoma:
إِن تُرِيدُ إِلَّا أَن تَكُونَ جَبَّارًا فِي الْأَرْضِ
”Hutaki lolote isipokuwa uwe jabari katika nchi.”[3]?
[1] at-Tirmidhiy (2000), ambaye amesema kuwa ni nzuri na ngeni. Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (2000).
[2] 26:130
[3] 28:19
- Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 248-253
- Imechapishwa: 26/03/2026

Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 248-253
Imechapishwa: 26/03/2026
https://firqatunnajia.com/29-basi-wewe-ni-dhalimu/