Ni jambo la kusikitisha kuwa wengi katika waislamu wameacha kutumia tarehe ya Hijriyyah na kuchukua tarehe ya kikristo ya Miladiy ambayo imejengwa juu ya miezi ya kubuni, isiyo na msingi wa Kishari´ah, kiakili wala wa kihisia. Hili linaonyesha udhaifu, kushindwa na kuwafuata wasio waislamu. Miongoni mwa maovu yake ni kuwaunganisha waislamu na kizazi chao kipya na historia ya wakristo na kuwafanya waepukane na historia yao ya Hijrah iliyoambatana na Mtume wao (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), alama za dini yao na ´ibaadah zao[1].
Hadiyth inafahamisha kwamba swawm bora ya kujitolea baada ya Ramadhaan ni swawm ya mwezi wa Allaah Muharram. Dhahiri ni kwamba huu ndio mwezi bora kabisa wa kujitolea kufunga baada ya Ramadhaan. Hata hivyo kufunga baadhi ya siku ndani ya miezi mingine kunaweza kuwa bora zaidi, kama siku ya ´Arafah na siku sita za Shawwaal.
Maana ya wazi ya Hadiyth ni kwamba kufunga mwezi mzima wa Muharram ni jambo lenye fadhilah, ingawa baadhi ya wanazuoni wameielewa Hadiyth hii kuwa ni kuhamasisha tu kufunga siku nyingi za mwezi wa Muharram na si kwamba mtu afunge mwezi mzima. Hilo ni kutokana na maneno yake ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa):
“Sijapatapo kumuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akitimiza swawm ya mwezi mzima kamwe isipokuwa Ramadhaan na sijapatapo kumuona akifunga sana ndani ya mwezi mwingine kama alivyofunga Sha´baan.”[2]
Ameipokea Muslim.
[1] Tazama ”Tashabbuh-ul-Manhiyy ´anh”, uk. 542.
[2] Muslim (1156) na (175).
- Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 52-53
- Imechapishwa: 15/05/2025
Ni jambo la kusikitisha kuwa wengi katika waislamu wameacha kutumia tarehe ya Hijriyyah na kuchukua tarehe ya kikristo ya Miladiy ambayo imejengwa juu ya miezi ya kubuni, isiyo na msingi wa Kishari´ah, kiakili wala wa kihisia. Hili linaonyesha udhaifu, kushindwa na kuwafuata wasio waislamu. Miongoni mwa maovu yake ni kuwaunganisha waislamu na kizazi chao kipya na historia ya wakristo na kuwafanya waepukane na historia yao ya Hijrah iliyoambatana na Mtume wao (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), alama za dini yao na ´ibaadah zao[1].
Hadiyth inafahamisha kwamba swawm bora ya kujitolea baada ya Ramadhaan ni swawm ya mwezi wa Allaah Muharram. Dhahiri ni kwamba huu ndio mwezi bora kabisa wa kujitolea kufunga baada ya Ramadhaan. Hata hivyo kufunga baadhi ya siku ndani ya miezi mingine kunaweza kuwa bora zaidi, kama siku ya ´Arafah na siku sita za Shawwaal.
Maana ya wazi ya Hadiyth ni kwamba kufunga mwezi mzima wa Muharram ni jambo lenye fadhilah, ingawa baadhi ya wanazuoni wameielewa Hadiyth hii kuwa ni kuhamasisha tu kufunga siku nyingi za mwezi wa Muharram na si kwamba mtu afunge mwezi mzima. Hilo ni kutokana na maneno yake ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa):
“Sijapatapo kumuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akitimiza swawm ya mwezi mzima kamwe isipokuwa Ramadhaan na sijapatapo kumuona akifunga sana ndani ya mwezi mwingine kama alivyofunga Sha´baan.”[2]
Ameipokea Muslim.
[1] Tazama ”Tashabbuh-ul-Manhiyy ´anh”, uk. 542.
[2] Muslim (1156) na (175).
Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 52-53
Imechapishwa: 15/05/2025
https://firqatunnajia.com/28-swawm-bora-kabisa-baada-ya-ramadhaan/