Pengine wengine wakajaribu kuleta hoja kwa maneno Yake (Subhaanahu wa Ta´ala) pale alipomwamrisha Muusa (´alayhis-Salaam):
إِنِّي أَنَا رَبُّكَ فَاخْلَعْ نَعْلَيْكَ ۖ إِنَّكَ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى
”Hakika mimi ni Mola wako! Hivyo vua viatu vyako; hakika wewe uko katika bonde takatifu la Twuwaa.”[1]
Utumiaji dalili huu uko mbali kabisa. Allaah amrehemu Ibn Mas’uud alipomwambia Abu Muusa al-Ash’ariy wakati alipowaswalisha kisha akavua viatu vyake:
“Kwa nini umevua viatu vyako? Je, wewe uko kwenye bonde Twuwaa?”[2]
Abu Muhammad bin Hazm (Rahimahu Allaah) amesema:
”Miongoni mwa Shari´ah za Muusa (´alayhis-Salaam) ni maneno Yake (Ta´ala):

”Hakika mimi ni Mola wako! Hivyo vua viatu vyako; hakika wewe uko katika bonde takatifu la Twuwaa.”
Hata hivyo sisi hatuvui viatu vyetu katika ardhi takatifu.”[3]
Anachokusudia (Rahimahu Allaah) ni kwamba sisi hatukuwajibishwa kufuta Shari´ah za waliokuwa kabla yetu. Vinginevyo sijui kama kuna hoja tata nyingine muhilo inayopaswa kutaja. Kuhusu dhana za wajinga na yale wanayoonelea kuwa ni mazuri, njia pekee ya kuyaondoa ni wanazuoni kuifanyia kazi Sunnah. Wakati watu wa kawaida wanapowaona wanazuoni wanaifanyia kazi Sunnah, basi nao wataifanyia kazi.
[1] 20:12
[2] ´Abdur-Razzaaq (1/386) na Ibn Abiy Shaybah (2/418). Wanaume wake ni wanaume Swahiyh.
[3] al-Ihkaam fiy Usuul-il-Ahkaam.
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 32
- Imechapishwa: 23/06/2025
Pengine wengine wakajaribu kuleta hoja kwa maneno Yake (Subhaanahu wa Ta´ala) pale alipomwamrisha Muusa (´alayhis-Salaam):
إِنِّي أَنَا رَبُّكَ فَاخْلَعْ نَعْلَيْكَ ۖ إِنَّكَ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى
”Hakika mimi ni Mola wako! Hivyo vua viatu vyako; hakika wewe uko katika bonde takatifu la Twuwaa.”[1]
Utumiaji dalili huu uko mbali kabisa. Allaah amrehemu Ibn Mas’uud alipomwambia Abu Muusa al-Ash’ariy wakati alipowaswalisha kisha akavua viatu vyake:
“Kwa nini umevua viatu vyako? Je, wewe uko kwenye bonde Twuwaa?”[2]
Abu Muhammad bin Hazm (Rahimahu Allaah) amesema:
”Miongoni mwa Shari´ah za Muusa (´alayhis-Salaam) ni maneno Yake (Ta´ala):
إِنِّي أَنَا رَبُّكَ فَاخْلَعْ نَعْلَيْكَ ۖ إِنَّكَ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ طُوًى
”Hakika mimi ni Mola wako! Hivyo vua viatu vyako; hakika wewe uko katika bonde takatifu la Twuwaa.”
Hata hivyo sisi hatuvui viatu vyetu katika ardhi takatifu.”[3]
Anachokusudia (Rahimahu Allaah) ni kwamba sisi hatukuwajibishwa kufuta Shari´ah za waliokuwa kabla yetu. Vinginevyo sijui kama kuna hoja tata nyingine muhilo inayopaswa kutaja. Kuhusu dhana za wajinga na yale wanayoonelea kuwa ni mazuri, njia pekee ya kuyaondoa ni wanazuoni kuifanyia kazi Sunnah. Wakati watu wa kawaida wanapowaona wanazuoni wanaifanyia kazi Sunnah, basi nao wataifanyia kazi.
[1] 20:12
[2] ´Abdur-Razzaaq (1/386) na Ibn Abiy Shaybah (2/418). Wanaume wake ni wanaume Swahiyh.
[3] al-Ihkaam fiy Usuul-il-Ahkaam.
Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: as-Swalaah fiyn-Ni´aal, uk. 32
Imechapishwa: 23/06/2025
https://firqatunnajia.com/28-muusa-alivua-viatu-vyake-sisi-hatufanyi-hivo/