Hakika swawm ni miongoni mwa ´ibaadah zenye manufaa makubwa zaidi na athari zake ni pana sana katika kuitakasa nafsi na kurekebisha maadili. Aidha ina faida nyingi adhimu. Miongoni mwa faida zake kubwa zaidi ni zifuatazo:
1 – Swawm ni sababu ya kupandikiza uchaji Allaah ndani ya nyoyo na kuzizuia viungo dhidi ya yaliyo haramu. Allaah (Ta´ala) amesema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ
“Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa kufunga kama ilivyofaradhishwa kwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Allaah.”[1]
Amebainisha (Subhaanha) ndani ya Aayah hii kuwa ameweka Shari´ah ya funga kwa waja Wake ili wawafikishwe kumcha Allaah. Uchaji Allaah ni neno linalokusanya sifa zote za kheri. Allaah amefungamanisha kheri nyingi na matunda mengi na uchaji na ameitaja mara nyingi katika Qur-aan kwa sababu ya umuhimu wake. Wanazuoni wameifasiri uchaji kuwa ni kutekeleza amri za Allaah na kujiepusha na makatazo Yake kwa matarajio ya thawabu Zake na kwa kuogopa adhabu Yake. Kuhusu maneno Yake (Ta´ala):
لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ
“… ili mpate kumcha Allaah.”
Imaam al-Qurtwubiy (Rahimahu Allaah) amesema:
”Neno (لعل) hapa ni matarajio kwa upande wao na mpate kumcha Allaah maana yake ni muache maasi, kwani kadiri kula kunavyopungua ndivyo matamanio yanavyodhoofika, na kadiri matamanio yanavyodhoofika ndivyo maasi yanavyopungua. Pia imeelezwa kuwa maana yake ni ya ujumla, kwa kuwa swawm ni kinga na ni kukata matamanio, kama alivosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Swawm ni kinga na ngao.”[2]
2 – Miongoni mwa faida za swawm ni kwamba humzoesha mtu subira, uvumilivu na uimara, kwa sababu humlazimisha kuacha aliyozoea na kujitenga na matamanio yake kwa kutaka kwake na kuridhia. Humpa nguvu muislamu namna hii aliyekuwa amezowea maasi ili aweze kuyaacha na kujiepusha nayo. Swawm humlea kwa malezi ya kivitendo juu ya subira dhidi ya maasi na kuyasahau mpaka anayatelekeza kabisa. Mfano wake ni mvutaji sigara ambaye tabia hiyo imemshinda na ikawa vigumu kwake kuiacha kupitia swawm anaweza kuacha tabia hiyo mbaya na kitu hicho kichafu kwa urahisi. Vivyo hivyo kwa maasi mengine yote.
[1] 02:183
[2] Ahmad (02/257) (nr. 402) (04/22), an-Nasaa’iy (2227, 2229), Ibn Maajah (1639), at-Twabaraaniy (08/157-158) (nr.7608).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 30-31
- Imechapishwa: 23/02/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 30-31
Imechapishwa: 23/02/2026
https://firqatunnajia.com/28-miongoni-mwa-faida-za-swawm/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket