192 – ´Abdur-Rahmaan bin Swaalih ametuhadithia: Abu Bakr bin ´Ayyaas ametuhadithia: kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa ´Alqamah, kutoka kwa ´Abdullaah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Hataingia Peponi mtu ambaye moyoni mwake mna uzito wa chembe ya haradali ya kiburi, wala hataingia Motoni mtu ambaye moyoni mwake mna uzito wa chembe ya haradali ya imani.”[1]

193 – Abu ´Ammaar al-Husayn bin Hurayth ametuhadithia: al-Fadhwl bin Muusa ametuhadithia, kutoka kwa al-Husayn bin Waaqid, kutoka kwa Yahyaa bin ´Aqiyl: Nimemsikia ´Abdullaah bin Abiy Awfaa akisema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anakithirisha Dhikr na kupunguza upuuzi, na hakuwa akijivuna kutembea na mjane na masikini akamtimizia haja yake.”[2]

194 – Abu Khaythamah ametuhadithia: ´Affaan ametuhadithia: Hammaad bin Salamah ametuhadithia, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas, aliyesema:

”Mwanamke mmoja alikuwa na upungufu katika akili yake, akasema: ”Ee Mtume wa Allaah, hakika mimi nina haja.” Akasema: ”Ee mama wa fulani, angalia njia ipi utakayo. Akasimama pamoja naye akizungumza naye hadi akamtatulia haja yake.”[3]

195 – Ahmad bin Maniy´ ametuhadithia: Ibn ´Ulayyah ametuhadithia, kutoka kwa ´Ammaar (mpwa wa ath-Thawriy): ´Atwaa’ bin as-Saa-ib ametuhadithia, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesimulia ya kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

Allaah (´Azza wa Jall) anasema: ”Kiburi ni joho Langu na ukubwa ni kikoi Changu. Basi atakayenivuta katika mojawapo kati ya hivyo, nitamtupa ndani ya Jahannam.”[4]

196 – Ahmad bin Maniy´ ametuhadithia: Marwaan bin Shujaa´ ametuhadithia, kutoka kwa Ibraahiym bin Abiy ´Albah, kutoka kwa Abu Salamah bin ´Abdir-Rahmaan, ambaye amesema:

´Abdullaah bin ´Umar na ´Abdullaah bin ´Amr walikutana kwa al-Marwah, ambapo Ibn ´Amr akaendelea na Ibn ´Umar akabaki analia. Akasema: ”Ni nini kinakububujisha machozi, ee Abu ´Abdir-Rahmaan?” Huyu – akimaanisha Ibn ´Amr – anadai kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: ”Atakayekuwa moyoni mwake kuna uzito wa chembe ya haradali ya kiburi, basi Allaah atamwangusha kifudifudi ndani ya Moto.”[5]

197 – Yahyaa bin ´Abdil-Majiyd al-Hummaaniy ametuhadithia: Ja´far bin Sulaymaan “

”Nabii (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipita katika njia, na mwanamke mweusi akapita. Bwana mmoja akamwambia mwanamke yule: ”Iko wapi njia?” Mwanamke yule akasema: ”Njia iko pale.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Achana naye, hakika yeye ni mwenye kiburi.”[6]

[1] Muslim (147-149).

[2] an-Nasaa’iy (1413). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan an-Nasaa’iy” (1413).

[3] Muslim (2326).

[4] Abu Daawuud (4090). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (4090).

[5] Wapokezi wake ni wapokezi wa Swahiyh kwa mujibu wa al-Haythamiy katika “Majma´-uz-Zawaa’id” (1/98).

[6] al-Haythamiy amesema:

“Ahmad ameidhoofisha na ametuhumiwa uwongo na Yahyaa al-Hummaaniy.” (Majma´-uz-Zawaa’id” (1/99))

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 241-247
  • Imechapishwa: 25/03/2026