Haafidhw Abu Nu’aym (Rahimahu Allaah) amesema katika kitabu chake “Asmaa’-us-Swahaabah” amesimulia kutoka kwa Shaykh Abu Sulaymaan ad-Daaraaniy (Rahimahu Allaah), ambaye amesema: ´Alqamah bin Suwayd bin al-Haarith al-´Azdiy amenihadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba yake, ambaye ameeleza kwamba Luqmaan mwenye hekima alimwambia mwanawe:
“Nimekukusanyia hekima yangu katika sentensi sita: Ifanyie kazi dunia yako kulingana na muda wako wa kubaki huko. Ifanyie kazi Aakhirah kulingana na muda wako wa kubaki huko. Mfanyie kazi Allaah kulingana na kule kumuhitajia kwako. Yafanyie kazi madhambi kulingana na subira yako ya kuvumilia adhabu. Usimuulize isipokuwa tu yule asiyemuhitajia yeyote. Ukitaka kumuasi Allaah, basi muasi pale Yeye hawezi kukuona.”
Ibraahiym al-Khawwaasw (Rahimahu Allaah) amesema:
“Dawa za moyo ni mambo matano: Kusoma Qur-aan kwa mazingatio, tumbo tupu, kusimama usiku kuswali, unyenyekevu katika nyakati za mwishoni mwa usiku na kukaa na waja wema.”
Wakati wa maneno Yake Allaah (Ta’ala):
وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ
“Mola wenu Amesema: “Niombeni, Nitakuitikieni.”[1]
kulisemwa kuambiwa Ibraahiym bin Ad-ham (Rahimahu Allaah): “Tunamwomba lakini hatuitikii.” Ndipo akawaambia: “Mmemjua Allaah lakini hamumuitikii. Mmesoma Qur-aan lakini hamkuifanyia kazi. Mmemjua shaytwaan na mkaenda sambamba naye. Mnadai kumpenda Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) na mkaiacha njia yake. Mnadai kuipenda Pepo na hamuifanyii kazi kimatendo. Mnadai kuogopa Moto na hamwachi kufanya madhambi. Mnasema kuwa kifo ni haki na wala hamjiandai nacho. Mnajishughulisha na mapungufu ya wengine na hamjishughulishi na mapungufu yenu. Mnakula riziki ya Allaah na hamumshukuru kwayo. Mnawazika wafu wenu na wala hampati mazingatio kwayo.”[2]
Tunamuomba Allaah atuwafikishe kwa yale anayoyaridhia kwetu kwa rehema Zake na atujaalie mwisho mwema. Aamiyn. Hakika Yeye ndiye Mwingi wa kurehemu kuliko wenye kurehemu wote, Mola wa walimwengu wote. Ee Allaah (Ta´ala) msifu Mtume wa mwisho, bwana wetu Muhammad, jamaa zake na Maswahabah zake wote. Allaah ni Mwenye kunitosheleza; Naye ndiye mbora wa kutegemewa.
[1] 40:60
[2] Hilyat-ul-Awliyaa (8/15).
- Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 106-109
- Imechapishwa: 24/11/2025

Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 106-109
Imechapishwa: 24/11/2025
https://firqatunnajia.com/28-hekima-zake-luqmaan/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket