Wakanushaji wanategemea utata batili[1]. Kila ambaye Allaah amemtunuku elimu sahihi na uelewa sahihi anajua ni shubuha batilifu. Wanategemea vidhibiti vifuatavyo:
1- Madai batilifu kama kudai kwamba wanasapotiwa na maafikiano au kwamba maoni yao yamehakikishwa au kwamba maoni yao ndio ya wale wanachuoni wahakikishaji au kwamba maoni ya wapinzani wao yanaenda kinyume na maafikiano na mfano wa hayo.
2- Utata uliopandana na kipimo ambacho ni kibovu. Kwa mfano wanasema kuwa kuthibitisha sifa kunalazimisha ufananisho. Wanasema kuwa sifa ni aradhi na aradhi haiwezi kusimama pekey ake isipokuwa mpaka kwa kiwiliwili na viwiliwili ni vyenye kufanana.
3- Wanashikilia matamshi yenye kushirikiana ambayo yanaweza kunasibishwa kwa Allaah na kutonasibishwa. Mfano wa ibara hizo ni kama kiwiliwili, mpaka na upande. Wanatumia matamshi kama haya ya kijumla na kusema kuwa Allaah hasifiwi nayo ili kufikia kwamba hasifiwi kwa sifa Zake.
Isitoshe wanaunda shubuha hizi kwa ibara za kupambapamba, ndefu na za ajabu ambazo mjinga anaweza kufikiria kuwa ni haki. Pindi atapokagua jambo hili, ataona kuwa si jengine zaidi ya shubuha batili. Watu hawa wanaraddiwa ifuatavyo:
1- Shubuha na utata wao ni wenye kujigonga kwa sababu kile wanachokithibitisha kinalazimisha yale wanayoyakimbia pindi wanapokanusha.
2- Maoni yao ni yenye kujigonga kwa sababu kila pote katika wao linamaanisha kuwa akili inalazimisha hilo ilihali akili ya pote lingine inakipinga. Huenda mmoja wao akasema kitu ambacho anadai kuwa ni chenye kulazimishwa na akili halafu baada ya muda mfupi akasema kinyume chake. Mgongano wa maoni ni dalili moja wapo yenye nguvu kabisa kuonyesha kuwa ni batili.
3- Malazimisho yao batilifu ya ukanushaji yanatakiwa kubainishwa. Lazimisho batili linajulisha ubatilifu wa kile chenye kulazimishwa.
4- Maandiko yaliyothibiti juu ya sifa hayawezi kufahamika vyengine zaidi ya udhahiri wake. Endapo andiko fulani litafahamika vyengine, haina maana kwamba haliwezi kufasiriwa udhahiri wake. Kwa vile hakuna chenye kuzuia kulifasiri udhahiri wake, ni lazima kuliendea.
5- Ni jambo linalojulikana fika kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye ambaye alifikisha masuaha haya ya sifa. Hivyo kuyapotosha ndio mtindo uleule wa upotoshaji wa Qaraamitwah na Baatwiniyyah juu ya swalah, swawm, hajj na mengineyo.
6- Akili timamu haionelei kuwa ni jambo lisilowezekana kuamini sifa za Allaah. Uhakika wa mambo ni kwamba akili timamu inafahamisha juu ya kuthibitisha sifa za Allaah kikamilifu. Hata hivyo katika suala hili kuna mambo ya kina ambayo akili haiwezi kuyafahamu na kuyazunguka.
Vigogo wa watu hawa wamekiri wenyewe kuwa ni jambo lisilowezekana kwa akili kuhakikisha masuala ya kiungu. Kujengea juu ya hili ni lazima kupokea suala hili kutokaba katika ulinganizi wa kiutume pasi na upotoshaji – na Allaah ndiye anajua zaidi.
[1] Miongoni mwayo ni maneno Yake (Ta´ala):
هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا
“Je, unamjua mwenye jina kama Lake?” (19:65)
وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ
“Na wala hana yeyote anayefanana [na kulingana] Naye.” (112:4)
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fath Rabb-il-Bariyyah, uk. 70-71
- Imechapishwa: 11/05/2020

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fath Rabb-il-Bariyyah, uk. 70-71
Imechapishwa: 11/05/2020
https://firqatunnajia.com/27-utata-wa-wakanushaji/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)