6- Imechukizwa kufunga siku za kuchinja. Nazo ni zile siku tatu baada ya ile siku ya ´Iyd-ul-Adhwhaa; siku ya tarehe kumi na moja,  tarehe kumi na mbili na tarehe kumi na tatu. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ni siku za kula, kunywa na kumtaja Allaah (´Azza wa Jall).”[1]

“Siku ya ´Arafah, siku  ya Nahr na siku za Tashriyq ni sikukuu zetu waislamu na pia ni siku za kula na kunywa.”[2]

Amemruhusu mwenye kufanya Tamattu´ na Qiraan wasipopata thamani ya kichinjwa. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya ´Aaishah na Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhum) waliosema:

“Hakuruhusu katika zile siku za Tashriyq kufunga isipokuwa kwa yule ambaye hakupata kichinjwa.”[3]

[1] Muslim (1141).

[2] at-Tirmidhiy (777) ambaye amesema:

”Nzuri na Swahiyh.”

Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Tirmidhiy” (620).

[3] al-Bukhaariy (1997, 1998).

  • Mhusika: Nukhbatin minal-´Ulamaa´
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fiqh-ul-Muyassar, uk. 166
  • Imechapishwa: 17/05/2020