Imekuja katika ”al-Miswbaah” ya kwamba ”soksi” (جورب) ni neno lililoingizwa katika kiarabu na ni wingi wake ni soksi (جواربة) au (جوارب)”. Hakulifafanua neno hilo kwa sababu ni lenye kufahamika kwa kila mmoja. Kilicho wazi hakihitaji utambulisho.”
Imekuja katika ”al-Qaamuus” ya kwamba soksi ni ”kifuniko cha mguu”, kama ilivyokuja pia katika ”Lisaan-ul-´Arab”.
Abu Bakr bin al-´Arabiy amesema kwamba soksi ni ”vifuniko viwili vya mguu vilivyotengenezwa kwa sufu ambavyo huvaliwa kwa ajili ya kujikinga na baridi”.
al-Hattwaab al-Maalikiy amesema katika ”at-Tawdhwiyh” ya kwamba soksi ni ”kile kilicho katika umbo la soksi za ngozi kilichotengenezwa kwa kitani, pamba au kinginecho.
al-Bahuutwiy al-Hanbaliy amesema katika ”ar-Rawdhw al-Murbiy” ya kwamba soksi ni ”kile kinachovaliwa mguuni kwa mfano wa soksi za ngozi kisichokuwa ngozi.
al-´Ayniy amesema ya kwamba soksi ni ”kile kinachovaliwa na watu wa nchi za Shaam zenye baridi kali, hutengenezwa kwa uzi wa sufu uliosokotwa, huvaliwa mguuni hadi juu ya vifundo”.
al-Halabiy amesema katika “Ghunyat-ul-Mutamalliy” soksi ni ”kile kinachovaliwa mguuni kwa ajili ya kuzuia baridi na mfano wake ambacho hakiitwi soksi za ngozi wala buti”.
Wanazuoni wamesema kuwa buti ni soksi za ngozi nene zinazovaliwa juu ya soksi za ngozi. Ibn Siydah amesema kwamba buti ni ”aina fulani ya soksi za ngozi”.
al-Jawhariy amesema kuwa buti ni ”aina ya soksi za ngozi zinazovaliwa juu ya soksi za ngozi”. Nazo ni neno la Kiajemi lililoingizwa katika Kiarabu.
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 50
- Imechapishwa: 09/04/2026
Imekuja katika ”al-Miswbaah” ya kwamba ”soksi” (جورب) ni neno lililoingizwa katika kiarabu na ni wingi wake ni soksi (جواربة) au (جوارب)”. Hakulifafanua neno hilo kwa sababu ni lenye kufahamika kwa kila mmoja. Kilicho wazi hakihitaji utambulisho.”
Imekuja katika ”al-Qaamuus” ya kwamba soksi ni ”kifuniko cha mguu”, kama ilivyokuja pia katika ”Lisaan-ul-´Arab”.
Abu Bakr bin al-´Arabiy amesema kwamba soksi ni ”vifuniko viwili vya mguu vilivyotengenezwa kwa sufu ambavyo huvaliwa kwa ajili ya kujikinga na baridi”.
al-Hattwaab al-Maalikiy amesema katika ”at-Tawdhwiyh” ya kwamba soksi ni ”kile kilicho katika umbo la soksi za ngozi kilichotengenezwa kwa kitani, pamba au kinginecho.
al-Bahuutwiy al-Hanbaliy amesema katika ”ar-Rawdhw al-Murbiy” ya kwamba soksi ni ”kile kinachovaliwa mguuni kwa mfano wa soksi za ngozi kisichokuwa ngozi.
al-´Ayniy amesema ya kwamba soksi ni ”kile kinachovaliwa na watu wa nchi za Shaam zenye baridi kali, hutengenezwa kwa uzi wa sufu uliosokotwa, huvaliwa mguuni hadi juu ya vifundo”.
al-Halabiy amesema katika “Ghunyat-ul-Mutamalliy” soksi ni ”kile kinachovaliwa mguuni kwa ajili ya kuzuia baridi na mfano wake ambacho hakiitwi soksi za ngozi wala buti”.
Wanazuoni wamesema kuwa buti ni soksi za ngozi nene zinazovaliwa juu ya soksi za ngozi. Ibn Siydah amesema kwamba buti ni ”aina fulani ya soksi za ngozi”.
al-Jawhariy amesema kuwa buti ni ”aina ya soksi za ngozi zinazovaliwa juu ya soksi za ngozi”. Nazo ni neno la Kiajemi lililoingizwa katika Kiarabu.
Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 50
Imechapishwa: 09/04/2026
https://firqatunnajia.com/27-soksi-ni-soksi/