Miongoni mwa fadhilah zake ni kwamba hufanya matendo yote ya mwenye kufunga kuwa ni ´ibaadah. Abu Daawuud at-Twayaalisiy na al-Bayhaqiy wamepokea kupitia kwa Ibn ´Umar kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:
”Swawm ya mwenye kufunga ni Tasbiyh, usingizi wake ni ´ibaadah, du´aa yake inakubaliwa na matendo yake yanazidishiwa thawabu.”[1]
Miongoni mwa fadhilah za swawm ni kwamba ni sehemu ya subira. at-Tirmidhiy na Ibn Maajah wamepokea ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Swawm ni nusu ya subira.”[2]
Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amekhabarisha ya kwamba wenye kusubiri watalipwa thawabu zao bila hesabu.
Miongoni mwa fadhilah na faida za kitabibu za swawm ni kwamba husababisha afya ya mwili. Imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Fungeni mtapata afya.”[3]
Hili ni kwa sababu funga inahifadhi viungo vya nje na vya ndani vya mwili na hulinda dhidi ya kuchanganya vyakula ovyo kunakosababisha maradhi. Kwa ujumla swawm ina faida nyingi sana ambazo haziwezi kuhesabiwa zote hapa. Lakini lengo ni kuashiria baadhi yake tu. Kwa kiwango hiki inatosha – Allaah akitaka.
[1] Daylamiy katika ”Musnad-ul-Firdaws” (3576), al-Hindiy katika ”Kanz-ul-´Ummaal” ambapo ameiegemeza kwa Abuz-Zakariyyaa bin Mandah (23602).
[2] Ahmad (04/260), al-Bayhaqiy (07/177) (nr. 3297) na Ibn Maajah (1745).
[3] as-Sunniy na Abu Nu´aym. Ameitaja al-Hindiy katika ”Kanz-ul-´Ummaal” (32605) na akaiegemeza kwa Ibn-us-Sunniy na Abu Nu´aym. Haafidhw al-´Iraaqiy amesema:
”Ameipokea at-Twabaraaniy katika ”al-Awsatw na Abu Nu´aym katika ”at-Twibb an-Nabawiy” kutoka katika Hadiyth ya Abu Hurayrah kwa cheni ya wapokezi dhaifu.” (Takhriyj-ul-Ihyaa´” (03/75)).
as-Swaghaaniy amesema:
”Ni Hadiyth iliyotungwa.”
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 29-30
- Imechapishwa: 22/02/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 29-30
Imechapishwa: 22/02/2026
https://firqatunnajia.com/27-miongoni-mwa-fadhilah-za-swawm-iii/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket