27. Kutanguliza kwa Mtume Aakhirah kabla ya dunia

Ahmad, au at-Tirmidhiy, kutoka kwa Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

“Mola wangu (‘Azza wa Jall) alinipa pendekezo la kunigeuzia bonde la Makkah kuwa dhahabu. Nikasema: ”Hapana, ee Mola.” Akasema mara tatu: “Ninachagua kushiba siku moja na kuwa na njaa siku nyingine. Ninapokuwa na njaa naelekea Kwako, na ninaposhiba nakushukuru.”

Mtambuzi mmoja amesema:

“Anayedai utumwa na akabaki na makusudio ni mwongo katika madai yake. Utumwa unasihi pale ambapo anatokomeza makusudio yake yote na akatekeleza makusudio ya Bwana Wake. Akaitwa jina alilompa na sifa zake zikawa alizompa. Akiitwa kwa jina lake, anajibu kwa niaba ya utumwa. Hivyo hana jina wala maelezo. Hamwitikii isipokuwa yule aliyemwita kwa namna inayofahamisha kuwa yeye ni mja wa Mola wake.”[1]

Akasoma mashairi kwa kusema:

Shauku yangu, ee ‘Amr, ni Zahraa’

anaitamubua mwenye kuisikia na mwenye kuiona

Usiniite jengine ila mtumwa wake

kwa maana hilo ndilo jina langu la kweli

Kuna mwingine aliyesema:

Nifanye nini na hitaji langu la mtu asiyefaa

kama mimi, ilihali siwezi hata kujitajirisha?

Ni hitaji langu kwa mali yako

ambaye anaweza kunifurahisha na kunihuzunisha

Ninakuja kwa kushangaza kwenye milango yake

na kusema ‘Mlinzi wangu!’

Usiniite jengine isipokuwa mtumwa wake

kwa maana ndilo jina langu tukufu zaidi

[1] Ahmad (5/524) na at-Tirmidhiy (2347), ambaye amesema kuwa Hadiyth ni nzuri. Dhaifu kwa mujibu wa  al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (2347).

  • Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Hanbaliy (afk. 795)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Khushuu´ fiys-Swalaah, uk. 103-105
  • Imechapishwa: 24/11/2025