176 – ´Abdullaah bin Abiy Badr amenihadithia: Muhammad bin ´Ubayd ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin Abiy Saarah, kutoka kwa al-Hasan bin ´Aliy, ambaye amesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika Allaah (´Azza wa Jall) humpa mja malipo mja kutokana na tabia njema kama anavyompa yule anayepigana jihaad katika njia Yake, humjia thawabu asubuhi na jioni.”
177 – Muhammad bin al-Husayn amenihadithia: Yaziyd bin Haaruun ametuhadithia: Daawuud bin Abiy Hind ametuhadithia, kutoka kwa Mak-huul, kutoka kwa Abu Tha´labah al-Khushaniy, ambaye amesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika wale wenye kupendwa zaidi kwangu miongoni mwenu na waliokaribu zaidi na mimi katika kikao siku ya Qiyaamah ni wenye tabia njema zaidi. Hakika wale wenye kuchukiwa zaidi kwangu miongoni mwenu na walio mbali zaidi na mimi katika kikao siku ya Qiyaamah ni wenye tabia mbovu zaidi, wapiga porojo, wanaojivuta maneno na wenye majivuno katika maneno.”
178 – Ibraahiym bin Sa´iyd amenihadithia: Yuunus bin Muhammad ametuhadithia: Abu Uways ametuhadithia, kutoka kwa Muhammad bin al-Munkadir, kutoka kwa Jaabir, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Je, ni sikwambieni ni nani aliye kamilika zaidi katika imani yenu? Ni wenye tabia njema zaidi, wapole, wanaopatana na kupatanishwa.”
179 – Muhammad bin al-Husayn amenihadithia: Rawh bin ´Ubaadah ametuhadithia: ´Uthmaan bin Ghiyaath ametuhadithia: ´Abdullaah bin Shafiyq ametuhadithia:
”Kuna mtu alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akasema: ”Ee Mtume wa Allaah, kitu gani kilicho bora zaidi?” Akasema: ”Maadili mema.” Alisema hivo mara mbili au tatu.”
180 – Muhammad bin al-Husayn amenihadithia: Abu Nadhwr Haashim bin al-Qaasim ametuhadithia: al-Layth bin Sa´d ametuhadithia, kutoka kwa Zayd bin ´Abdillaah bin Usaamah, kutoka kwa Bakr bin al-Furaat, aliyesimulia ya kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Umbo la mtu na tabia yake kamwe haikuwa njema kisha likaliwa na Moto.”
181 – Abu Muhammad al-Bazzaar ametuhadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa al-Muttwalib bin Ziyaad, kutoka kwa ´Abdul-Malik bin ´Umayr, ambaye amesema:
”Hakika Allaah (´Azza wa Jall) anapompenda mja, basi humfanya mzuri wa umbo na mzuri wa tabia.”
182 – Abu Khaythamah ametuhadithia: Muslim bin Ibraahiym ametuhadithia: Swadaqah bin Muusa ametuhadithia … Pia Muhammad bin al-Husayn amenihadithia: Fahd bin Hayyaan ametuhadithia, kutoka kwa Swadaqah bin Muusa: Maalik bin Diynaar ametuhadithia: ´Abdullaah bin Ghaalib al-Huddaaniy ametuhadithia, kutoka kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy, aliyesimulia ya kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Sifa mbili hazikusanyiki kwa muumini: ubakhili na tabia mbaya.”
183 – ´Abdullaah bin Abiy Badr ametuhadithia: ´Abdul-Majiyd bin Abiy Rawwaad ametukhabarisha, kutoka kwa Marwaan bin Saalim, kutoka kwa bwana mmoja kutoka katika watu wa kisiwa, kutoka kwa Maymuun bin Mihraan, aliyesimulia ya kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakuna dhambi iliyo kubwa zaidi mbele ya Allaah (´Azza wa Jall) kuliko tabia mbaya. Hilo ni kwa sababu mwenye sifa hiyo hatoki katika dhambi isipokuwa huingia katika nyingine.”
- Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 225-233
- Imechapishwa: 25/03/2026

Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 225-233
Imechapishwa: 25/03/2026
https://firqatunnajia.com/26-uzuri-wa-ndani-na-wa-nje/