Shubuha ya tano ni yale yaliyopokelewa kuhusu Hadiyth ya Abu Muusa al-Ash´ariy. Abu Daawuud amesema katika ”as-Sunan” yake:
”Imepokelewa licha ya kwamba si yenye kuungana wala yenye nguvu.”[1]
as-Sindiy amesema katika maelezo yake juu ya Abu Daawuud:
”Kusema kwamba ”si yenye kuungana” ni kwa sababu ni katika mapokezi ya adh-Dhwahhaak bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Abu Muusaa. Hata hivyo haijathibiti kusikia kutoka kwake. Kusema kwamba ”wala yenye nguvu” ni kwa sababu ni katika mapokezi ya ´Iysaa bin Sinaan, kutoka kwa adh-Dhwahhaak. Ahmad, Ibn Ma´iyn, Abu Zur´ah, an-Nasaa’iy na wengineo wamemdhoofisha.”
Haafidhw Ibn Hajar amesema:
”Hadiyth ya Abu Muusa iliyoashiriwa na Abu Daawuud ameipokea Ibn Maajah. Katika cheni yake kuna udhaifu na kukatika, kama alivyosema Abu Daawuud.”
Jibu ya shubuha hii ni yale aliyosema ´Allaamah ´Alaa’-ud-Din al-Maardiyniy kwamba kudhoofishwa kwa sababu ya kutothibiti kusikia kwa ´Iysaa bin Sinaan kutoka kwa Abu Muusa ni kutokana na madhehebu ya wale wanaoshurutisha kuthibiti kusikia ili cheni iwe imeungana. Amesema:
”Isitoshe Ibn Ma´iyn ameonelea kuwa Ibn Sinaan ni mwenye kuaminika na wengine wamemdhoofisha. at-Tirmidhiy amepokea kutoka kwa ´Iysaa bin Sinaan katika Hadiyth kuhusu swalah ya jeneza na akasema kuwa ni nzuri.”[2]
adh-Dhahabiy amesema kuhusu ´Iysaa bin Sinaan:
”Ni miongoni mwa ambao zinaandikwa Hadiyth zake… baadhi yao wamesema kuwa alikuwa na nguvu. al-´Ijliy amesema kwamba ”hana neno”.”[3]
Kwa ujumla, japokuwa wapo waliomdhoofisha, wapo pia ambao wameonea kuwa ni mwenye kuaminika. Miongoni mwa maimamu wapo wasioacha Hadiyth ya aliyedhoofishwa mpaka wakubaliane wote juu ya kuachwa kwake[4]. Haisemwi kwamba jeruhi la kikosi kikubwa cha wanazuoni hutangulizwa mbele ya kusifu, kwa sababu hilo limefungwa na sharti la kuwa jeruhi liwe limefafanuliwa wala lisiwe la jumla, na pia liwe limejengwa juu ya jambo la uhakika, si kwa njia ya jitihada, kama alivyosema Imaam Ibn Daqiyq-il-´Iyd na as-Suyuutwiy akanukuu kutoka kwake katika ”at-Tadriyb”. Kwa hiyo suala linahitaji umakini, kwani si la kuachwa bila mipaka, kama walivyofahamu makosa. Licha ya hayo Hadiyth inaweza kuungwa mkono na kutiwa nguvu kwa kupokelewa kwa njia nyingine kwa tamko lake au kwa maana yake. Hakika mapokezi ya Abu Muusa haya yamekuja kwa tamko lake katika Hadiyth ya al-Mughiyrah na kwa maana yake katika Hadiyth ya Thawbaan kuhusu vitambaa vinavyofunika miguu. Kwa msemo mwingine Hadiyth inakuwa ni nzuri kupitia zingine, kama ilivyo iliyo nzuri yenyewe kama yenyewe, na zote mbili hufanyiwa kazi na hujengewa hoja kwa mujibu wa yaliyomo ndani yake.
Kwa ujumla hata kama Hadiyth hizi zitapewa kasoro kwa chochote zilichopewa miongoni mwa kukatika au hali isiyo ya kawaida, basi imedhihirika kwa tuliyoyathibitisha kwamba miongoni mwazo kuna Swahiyh kwa kujitegemea, kwa mujibu wa at-Tirmidhiy, na miongoni mwazo kuna Swahiyh kutokana na zingine. Katika misingi imetanabahishwa kuwa Hadiyth yenye kasoro – ikitiwa nguvu na Hadiyth dhaifu nyingine, maneno au kitendo cha Swahabah, maneno ya wanazuoni wengi, kipimo, kusambaa kwake bila kupingwa au inafayiwa kazi na watu wa zama hizo, basi mkusanyiko huo huwa ni hoja. Kwa sababu kutokana na kuungana kwa udhaifu mbili hupatikana nguvu inayotoa dhana. Tazama ”Jam´-ul-Jawaamiy´” na maelezo yake katika utatifi wake wa Hadiyth ambayo kuna Swahabah anayekosekana katika cheni ya wapokezi. Allaah husema haki na ndiye anayeongoza njia.
[1] Abu Daawuud (159).
[2] al-Jawhar an-Naqiy fir-Radd ´alaal-Bayhaqiy.
[3] Miyzaan-ul-I´tidaal.
[4] Tadriyb-ur-Raawiy, uk. 113.
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 47-49
- Imechapishwa: 09/04/2026

Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 47-49
Imechapishwa: 09/04/2026
https://firqatunnajia.com/26-kivovyote-hadiyth-ya-kupangusa-juu-ya-soksi-imethibiti/