158 – Muhammad bin ´Awf ametuhadithia: Abul-Mughiyrah ametukhabarisha: Safwaan bin ´Amr ametukhabarisha, kutoka kwa Shurayh bin ´Ubaydillaah, ambaye amesimulia:

“Abu Maalik al-Ash’ariy alipokuwa anataka kukata roho alisema: “Ee kabila la Ash’ar! Hebu waliopo kati yenu wawafikishie wale wasiokuwepo! Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Utamu wa dunia ni uchungu wa Aakhirah.”[1]

[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (3155).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 38
  • Imechapishwa: 06/07/2025