7 – al-Bazzaar akasimulia kwa cheni ya wapokezi Swahiyh:
”Ibn ´Umar alikuwa akitawadha hali viatu vyake vikiwa miguuni mwake ambapo akavipangusa na akisema: ”Hivyo ndivyo nilivyomwona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akifanya.”
Haafidhw Haafidhw Ibn Hajar ameitaja katika “Kitaab-ud-Diraayah fiy Takhriyj Ahaadiyth-il-Hidaayah”. as-Suyuutwiy amesema:
”Abul-Hasan ´Aliy bin Muhammad bin ´Abdil-Malik bin al-Qattwaan, mtunzi wa ”al-Wahm wal-Iyhaam”, ameisahihisha Hadiyth ya Ibn ´Umar hii iliyotolewa katika ”al-Musnad” ya al-Bazzaar”.”[1]
8 – al-Bayhaqiy amesimulia kwa cheni ya wapokezi nzuri kutoka kwa Ibn ´Umar aliyesema:
”Nilimwona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akivaa – yaani viatu vya ngozi vilivyonyooshwa – ambapo akatawadha navyo na kuvipangusa.”[2]
Haafidhw Ibn Hajar ameitaja katika “Kitaab-ud-Diraayah fiy Takhriyj Ahaadiyth-il-Hidaayah”.
9 – al-Bukhaariy na Muslim walisimulia kutoka kwa ´Ubayd bin Jurayj, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Umar, ambaye amesema:
”Nilimwona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akivaa viatu vya ngozi vilivyonyooshwa ambavyo havina manyoya na akitawadha navyo. Hivyo basi nikapenda kuvikivaa.”
Maana ya kauli yake “akitawadha navyo” ni kwamba alikuwa akivipangusa, kama ilivyobainishwa na riwaya ya al-Bazzaar na al-Bayhaqiy zilizotangulia. Riwaya zinafasiriana zenyewe kwa zenyewe. Ama maneno ya al-Bukhaariy kwamba maana yake ni kuosha miguu ndani ya viatu, al-´Ayniy amenakili ya kwamba Haafidhw al-Ismaa´iyliy ameraddi tafsiri hiyo, kwa sababu inapingana na yale yaliyosimuliwa kutoka kwa Ibn ´Umar mwenyewe.
10 – ad-Daarimiy amepokea katika ”al-Musnad” yake kutoka kwa ´Abdul-Khayr aliyesmea:
”Nilimwona ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) akitawahda na akapangusa juu ya viatu viwili vilivyo wazi, kisha akasema: ”Lau si kwa sababu nilimwona Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akifanya kama mlivyoniona mimi nikifanya, basi ningeliona chini ya nyayo kuwa ndilo lenye haki zaidi ya kupanguswa kuliko juu yake.”[3]
11 – Ibn Khuzaymah amepokea kwa njia ya ´Abdul-Khayr ambaye ameeleza:
”´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) aliomba chombo cha maji, kisha akatawadha wudhuu´ mwepesi na akapangusa juu ya viatu vyake[4]. Kisha akasema: ”Hivi ndivyo wudhuu´ wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa aliye twahara maadamu hajapatwa na hadathi.”[5]
Ibn Hibbaan alimfuata katika hilo na akasema kuhusu Hadiyth ya Aws iliyotangulia:
”Hili lilikuwa katika twaharah ya kujitolea.”[6]
Masimulizi yote haya yanafahamisha kwamba kupangusa juu ya viatu kulikuwa ni juu ya viatu vyenyewe tu, bila kuambatana na kitu kingine pamoja navyo kama soksi. Zote kwa pamoja zinaifasiri Hadiyth ya al-Mughiyrah kwa tuliyoyataja kabla. Kwa sababu hiyo wamekubaliana kutokuweka sharti la kuwepo kwa viatu juu ya soksi na wamejuzisha soksi kuwa nzito hata kama hazina soli, kama itakavyokuja. Hivyo hoja ya an-Naysaabuuriy na ya wengine pia ikaanguka.
[1] Tadriyb-ur-Raawiy, uk. 46.
[2] as-Sunan al-Kubraa (1/287) kupiita kwa Ibn Khuzaymah, ambaye pia ameipokea katika ”as-Swahiyh” yake (199) kwa cheni yake ya wapokezi Swahiyh, kama nilivyosema katika maelezo yangu juu yake. Niongeze hapa niseme: ”Ina njia nyingine pia kutoka kwa Ibn ´Umar inayofanana na riwaya ya al-Bazzaar. Ameipokea at-Twahaawiy katika ”Sharh-ul-Ma´aaniy” (1/97). Wapokezi wake ni wenye kuaminika na wanaojulikana isipokuwa Ahmad bin al-Husayn al-Lahabiy. Kuna nyingine yenye kuitia nguvu iliyosimuliwa na Ibn ´Abbaas, ambaye amesema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitawadha kwa kuosha kila kiungo chake mara mojamoja na akapangusa juu ya viatu vyake.”
Ameipokea ´Abdur-Razzaaq katika ”al-Muswannaf” (783) na al-Bayhaqiy (1/286) kupitia njia mbili, kutoka kwa Zayd bin Aslam, kutoka kwa ´Atwaa bin Yasaar. Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh na iko juu ya masharti ya al-Bukhaariy na Muslim.
[3] Katika cheni yake yumo Abu Ishaaq as-Sabiy´iy. Hakuwa na […] pamoja na kuchanganyikiwa kwake. Ameipokea ´Abdul-Khayr kwa njia ya kutoweka wazi amesikia kutoka kwa nani. Khaalid bin ´Alqamah al-Hamadaaniy, ambaye ni mwenye kuaminika, ameipokea kwa njia tofauti na yake, nayo ni kwamba aliosha mguu wake wa kulia mara tatu na mguu wake wa kushoto mara tatu. Ameipokea Abu Daawuud na wengineo kwa cheni ya wapokezi Swahiyh. Ibn Hibbaan pia ameisahihisha (150). Nimeitaja katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud”.
[4] Katika ile ya asili imekuja ”miguu yake”. Usahihi umefanyika kutokana na tamko la Ibn Khuzaymah.
[5] Katika cheni kwa Ibn Khuzaymah (200) yupo mpokezi aliyeachwa, lakini amepata mfuatiliaji kama nilivyobainisha katika maelezo yangu juu yake. Ibn Khuzaymah ameipokea pia katika ”as-Swahiyh” (202) na vivyo hivyo an-Nasaa’iy na Ibn Hibbaan kwa njia nyingine kutoka kwa ´Aliy. Lakini kwa tamko lisemalo ”miguu yake” badala ya ”viatu vyake”. Tayari umeshajua hapo kabla (152). Cheni yake ya wa pokezi ni Swahiyh juu ya masharti ya al-Bukhaariy, ambaye naye ameipokea katika ”as-Swahiyh” lakini bila ya kutaja wazi kupangusa.
[6] Wudhuu´ huu ulikuwa wa kujitolea na si kwa wajibu, kwa sababu haukuwa unatokana na wudhuu´ uliyochenguka, kama ambavyo Ibn Khuzaymah alivyoiwekea kichwa cha khabari. Kichwa chake cha khabari kiko wazi kabisa. Lakini imesihi kutoka kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba alipangusa juu ya viatu vyake katika wudhuu´ wa lazima baada ya kupatwa na hadathi, kama itakavyokuja. Hivyo basi inapaswa kuifahamu Hadiyth hii kuwa ni ya aliye twahara, si kwa sababu alipangusa juu ya viatu, bali kwa sababu alitawadha mwepesi. Hili linaungwa mkono na kwmaba kuna tamko jingine linalosema kwamba ”alipangusa uso wake na mikono yake miwili”. Kupangusa huku hakujuzu katika faradhi kabisa. Basi hilo ndilo alilolikusudia pale aliposema:
”Hivi ndivyo wudhuu´ wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa aliye twahara.”
Na vipi iwezekane kuifasiri Hadiyth hii juu ya kupangusa viatu hali hilo limethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa njia nyingi bila kutofautisha kati ya wudhuu´ wa kujitolea na wa faradhi? Bali imethibiti hilo kutoka kwa mpokezi wa Hadiyth mwenyewe katika faradhi kwa matamko ya wazi. Nayo ni ile aliyoipokea at-Twahaawiy kutoka kwa Abu Dhibyaan, ambaye ameeleza:
”Alimwona ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) akikojoa akiwa amesimama, kisha akaomba maji ambapo akatawadha, akapangusa juu ya viatu vyake, kisha akaingia msikitini akavivua viatu vyake na akaswali.” (Sharh-ul-Ma´aaniy” (1/97))
Ameipokea pia ´Abdur-Razzaaq katika ”al-Muswannaf” (783–784), Ibn Abiy Shaybah (1/190) na al-Bayhaqiy (1/288) kupitia njia kadhaa kutoka kwa Abu Dhibyaan, naye ni al-Junaabiy al-Kuufiy. Alikuwa ni mwenye kuaminika na alikuwa ni mmoja katika wapokezi wa al-Bukhaariy na Muslim. Amefanyiwa ufuatiliaji na wengi kutoka kwa ´Aliy na hilo linaweza kupatikana katika “al-Muswannaf” ya ´Abdur-Razzaaq na ya Ibn Abiy Shaybah.
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 44-47
- Imechapishwa: 09/04/2026

Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 44-47
Imechapishwa: 09/04/2026
https://firqatunnajia.com/25-mtume-wa-allaah-alipangusa-juu-ya-viatu-vyake/