170 – Abu Muslim ´Abdur-Rahmaan bin Yuunus ametuhadithia: ´Abdullaah bin Idriys ametuhadithia: Baba yangu na mjomba wangu wamenihadithia, kutoka kwa babu yangu, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu jambo ambalo litawaingiza watu wengi Peponi, ambapo akajibu: “Kumcha Allaah na tabia njema.” Akaulizwa tena juu ya kitu ambacho kitawaingiza watu Motoni, ambapo akajibu: ”Venye tobo viwili: mdomo na utupu.”[1]

171 – ´Aliy bin al-Ja´d ametuhadithia: Zuhayr ametukhabarisha, kutoka kwa Ziyaad bin ´Ilaaqah, kutoka kwa Usaamah bin Shariyk, ambaye ameeleza:

”Nilikuwa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi wakaja kwake mabedui kutoka kila mahali. Wakasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Ni kheri gani bora aliyopewa mtu (au muislamu)?” Akasema: ”Tabia njema.”[2]

172 – Abu Khaythamah na wengine wametuhadithia: Sufyaan bin ´Uyaynah ametukhabarisha, kutoka kwa ´Amr bin Diynaar, kutoka kwa Ibn Abiy Mulaykah, kutoka kwa Ya´laa bin Mamlak, kutoka kwa Umm-ud-Dardaa’, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Hakuna kitu kilicho kizito zaidi katika mizani ya muumini kuliko tabia njema. Hakika Allaah (Ta´ala) anamchukia mchafu wa maneno na mwenye maneno machafu.”[3]

173 – Abu Khaythamah ametuhadithia: Wahb bin Jariyr ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia, kutoka kwa al-Qaasim bin Abiy Bazzah, kutoka kwa ´Atwaa’ al-Kaykhaaraaniy, kutoka kwa Umm-ud-Dardaa’, kutoka kwa Abud-Dardaa’, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Hakuna kitu kilicho kizito zaidi katika mizani kuliko tabia njema.”[4]

174 – Abu Khaythamah ametuhadithia: Wakiy´ ametuhadithia: al-A´mash ametuhadithia, kutoka kwa Abu Waa-il, kutoka kwa Masruuq, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr, ambaye ameeleza:

”Hakuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mchafu wala mwenye kujiingiza katika uchafu na alikuwa akisema: ”Miongoni mwa wabora wenu ni wale wenye tabia nzuri zaidi.”[5]

175 – ´Abdullaah bin Abiy Badr amenihadithia: Zayd bin al-Hubaab ametuhadithia, kutoka kwa Mu´aawiyah bin Swaalih: ´Abdur-Rahmaan bin Jubayr bin Nufayr amenikhabarisha, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa an-Nawwaas bin Sam´aan, ambaye ameeleza:

”Alimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu wema na dhambi. Akajibu: ”Wema ni uzuri wa tabia, na dhambi ni lile linalositasita ndani ya nafsi yako, hata wakikupatia fatwa watu na wakikupatia fatwa.”[6]

[1] Nzuri kwa mujibu al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Adab al-Mufrad” (294).

[2] al-Haakim (1/121), aliyeisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.

[3] at-Tirmidhiy (2002), ambaye amesema kuwa Hadiyth ni nzuri na Swahiyh. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (2002).

[4] at-Tirmidhiy (2003). Swahiyh kwa mujibuwa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (2003).

[5] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Adab al-Mufrad” (271).

[6] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Adab al-Mufrad” (295).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa (afk. 281)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Khumuul wat-Tawaadhwu´, uk. 217-225
  • Imechapishwa: 25/03/2026