Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
176 – Sisi tunajitenga mbali na wao na tunawazingatia kuwa ni wapotofu na wabaya – Allaah ndiye Mwenye kulinda na kuwafikisha.
MAELEZO
Sisi tunajitenga mbali na wao na tunawajengea uadui kwa ajili ya Allaah. Tunawachukia kwa sababu ni wapotofu na watu wa batili. Ni lazima kuwakata, kuwachukia na kuwaraddi wao na batili yao. Sisi tunajiweka mbali na ambaye anasema kuwa mapote yote yanakusanywa na neno Uislamu na kwamba ni lazma kuzifumbia macho tofauti hizi kwa sababu kila mmoja ana haki ya kuzungumza na kuona anavotaka. Fikira hii ni batili na khatari juu ya ummah. Uhuru wa kuzungumza na maoni umewekewa mpaka na Qur-aan, Sunnah na yale waliyokuwemo Salaf. Mapote yote yanayoenda kinyume yako Motoni – kundi pekee lililookoka ni lile linalofuata yale aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake.
Kwa kumalizia ni kwamba mtu daima ni kitu cha kukosea. Ulinzi, kuwafikishwa, matikisiko na nguvu ni mikononi mwa Allaah. Mtu asijiaminishe mikononi mwake uokozi, isipokuwa anatakiwa kumtegemea Allaah na kumukhofu.
Mpaka hapa kimemalizika kitabu hiki kifupi, lakini kilichobarikiwa, kilichokusanya sentesi kuu katika ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Tunamuomba Allaah atunufaishe kwacho, amlipe thawabu nyingi mtunzi kutokana yale aliyoyabainisha, aliyoyaweka wazi, aliyoyaandika na kuwatakia ummah mema. Allaah amjaze kheri na maimamu wengine wa waislamu.
Na Allaah ndiye mjuzi zaidi. Swalah, amani na baraka zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 267
- Imechapishwa: 27/05/2025
Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
176 – Sisi tunajitenga mbali na wao na tunawazingatia kuwa ni wapotofu na wabaya – Allaah ndiye Mwenye kulinda na kuwafikisha.
MAELEZO
Sisi tunajitenga mbali na wao na tunawajengea uadui kwa ajili ya Allaah. Tunawachukia kwa sababu ni wapotofu na watu wa batili. Ni lazima kuwakata, kuwachukia na kuwaraddi wao na batili yao. Sisi tunajiweka mbali na ambaye anasema kuwa mapote yote yanakusanywa na neno Uislamu na kwamba ni lazma kuzifumbia macho tofauti hizi kwa sababu kila mmoja ana haki ya kuzungumza na kuona anavotaka. Fikira hii ni batili na khatari juu ya ummah. Uhuru wa kuzungumza na maoni umewekewa mpaka na Qur-aan, Sunnah na yale waliyokuwemo Salaf. Mapote yote yanayoenda kinyume yako Motoni – kundi pekee lililookoka ni lile linalofuata yale aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake.
Kwa kumalizia ni kwamba mtu daima ni kitu cha kukosea. Ulinzi, kuwafikishwa, matikisiko na nguvu ni mikononi mwa Allaah. Mtu asijiaminishe mikononi mwake uokozi, isipokuwa anatakiwa kumtegemea Allaah na kumukhofu.
Mpaka hapa kimemalizika kitabu hiki kifupi, lakini kilichobarikiwa, kilichokusanya sentesi kuu katika ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Tunamuomba Allaah atunufaishe kwacho, amlipe thawabu nyingi mtunzi kutokana yale aliyoyabainisha, aliyoyaweka wazi, aliyoyaandika na kuwatakia ummah mema. Allaah amjaze kheri na maimamu wengine wa waislamu.
Na Allaah ndiye mjuzi zaidi. Swalah, amani na baraka zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake.
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 267
Imechapishwa: 27/05/2025
https://firqatunnajia.com/245-kujitenga-mbali-na-wazushi-na-watetezi-wao/